Header Ads

SERENGETI BOYS KUREJEA NCHINI KESHOKIKOSI cha timu ya vijana cha Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, kinatarajia kuingia nchini usiku wa kesho Jumanne kikitokea Shelisheli ambapo kilikokwenda kucheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya vijana wenzao wa taifa hilo.

Katika mchezo huo wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa Afrika kwa vijana wa umri huo itakayofanyika mwakani nchini Madagascar, Serengeti Boys iliibuka na ushindi wa mabao 6-0, juzi Jumamosi na kupita hatua hiyo ya mtoano kwa jumla ya mabao 9-0 kufuatia ushindi wa mabao 3-0 iliyoupata hapa nyumbani.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, ameliambia Championi Jumatatu, kikosi cha Serengeti Boys na msafara mzima unatarajiwa kuwasili Dar, saa 7:00 usiku wa Jumanne ambapo safari ya kutoka Shelisheli itaanza leo Jumatatu saa 11 jioni.
Serengeti itacheza dhidi ya Afrika Kusini katika hatua inayofuatia.

No comments