Header Ads

Shinda Simu Kali Mpya ya Tecno Camon C9 Kwa Kufanya Hivi


Kampuni Ya Tecno Mobile iliyozindua simu yake kali ya Camon C9 hivi karibuni ambayo kwa sasa inakimbiza kwa mauzo imekuja na shindano la kugawa simu bure kwa wateja wake na yeyote ambaye atafanikiwa katika vigezo vilivyowekwa ili kupata mshindi. Camon C9 ina uwezo wa hali ya juu katika kupiga picha, uwezo wa 4G LTE na teknolojia mbali mbali za kisasa ikiwemo uwezo wa kujaza watu wengi takribani 50 katika selfie na “make up” halisi ambayo itazipa picha zako muonekano wa tofauti wa kuvutia.
tecno
Pichani wateja walionunua Camon C9 wakioneshana sifa mbalimbali za simu hiyo mpya mara.
Akitoa ufafanuzi wa jinsi ya kushiriki shindano hilo, Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Bwana Bo Chen ameeleza kwamba shindano hili ni kwa watumiaji wa simu aina yoyote na mteja anachotakiwa kufanya ni kujiunga katika “challenge” na kufanya kile ambacho kinaelekezwa kisha kuweka katika mitandao ya kijamii akitumia #SeeLifeinC9 na #TecnoCamonC9.
image
Jinsi ya Kushiriki
Ili kushinda hakikisha unafanya “challenge” zote na unapoweka picha kwenye mitandao ya Facebook, Twitter na Instagram hakikisha unatumia hashtag hizi #SeeLifeinC9 na #TecnoCamonC9 na tag Tecno Tanzania. Washindi watapatikana kwa jumla ya idadi ya Likes, Retweets na Shares.
Challenge 9, ambazo zimetajwa hapa;
  • Piga Picha ukiwa kwenye mnara wowote wa Askari au mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
  • Piga picha ya Panorama ikionesha eneo kubwa au vitu vingi
  • Piga picha ukiwa umeruka angani (Picha haitakiwi kuonesha umegusa ardhi au kukanyaga kitu chochote)
  • Piga picha kuonesha uoto wa asili wa Tanzania
  • Piga picha kuonesha anga la Tanzania
  • Piga picha kuonesha maisha ya kila siku ya Tanzania
  • Piga picha kuonesha mazingira ya Tanzania nyakati za usiku
  • Piga picha za kuonesha usafiri unaotumika Tanzania
  • Piga picha ukionesha watu wa jamii ya Kitanzania
Shindano hili linafungwa Tarehe 31 Julai 2016 na washindi watatangazwa punde baada ya shindano kufungwa.
Kufahamu Zaidi; Tembelea kurasa zetu
au fuatilia hashtag #SeeLifeinC9 kwenye Instagram, Twitter na Facebook

No comments