• Latest News

  July 18, 2016

  Uhusiano wangu na Arsenal haujavunjika - Henry

  Thienry Henry, amesema bado anaipenda Arsenal, na kuondoka kwake kwenye benchi la ufundi la kikosi cha vijana siyo mwisho wa kuisaidia timu hiyo.
  Mshambuliaji huyo wa zamani Arsenal Thierry Henry amesema hana kinyongo na klabu hiyo baada ya kuacha kukifundisha kikosi cha vijana cha timu hiyo hivi karibuni.
  Henry mfungaji wa muda wote wa klabu ya Arsenal, aliacha kukinoa kikosi cha U-18, baada ya kuambiwa na Arsene Wenger achague kazi moja kati ya hiyo, au aendelee na uchambuzi wa soka kwenye kituo cha Skysports.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa, alisema kuwa bado anaipenda Arsenal na alichokuwa anakifanya kwenye kikosi cha vijana cha timu hiyo, ni kutafuta uzoefu wa kufundisha wakati huu akisubiri kupata leseni ya daraja A ya ukocha barani Ulaya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Uhusiano wangu na Arsenal haujavunjika - Henry Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top