Header Ads

Urafiki wa Kajala na Wema waanza kurejea taratibu, huu ni uthibitisho upo hapa

Urafiki wa Kajala na Wema waanza kurejea taratibu, huu ni uthibitisho
Miezi sita iliyopita, Wema Sepetu alikuwa na hasira na Kajala kiasi cha hata kuthubutu kusema hamjui.
“Mimi mtu ambaye sitaki kujiassociate naye namtoa kabisa ndio maana naweza nikakaa nikakuuliza Kajala ni nani? Huu sio muda wa kumzungumzia na kumpa airtime,” Wema alimuambia Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kilichoruka January mwaka huu.

Na sasa huenda Wema ameanza kuufungua moyo wake na kutafuta sehemu ndogo ili kumsamehe. Leo ni siku ya kuzaliwa ya Kajala na Wema ameungana na mastaa wengine kumpongeza muigizaji huyo.


Wema ametumia post tatu kwenye Snapchat kumpongeza Kajala.

Wawili hao waliwahi kuwa marafiki wakubwa miaka miwili iliyopita ambapo Wema alimlipia Kajala shilingi milioni 13 ya hukumu aliyopewa mahakamani kwa kesi iliyokuwa ikiwakabili na aliyekuwa mume wake.

No comments