Header Ads

Uwoya: Sipendi kudumu na mpenzi mmoja

 Staa wa filamu mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Irene Uwoya ametoa kali ya mwaka kwa kusema kuwa, huwa hana mzuka wa kudumu na mpenzi mmoja kwa muda mrefu akidai kuwa, wakizoeana sana inakuwa kero kwake.
 
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Uwoya alisema kuwa haoni sababu ya kukaa muda mrefu na mpenzi kwa sababu siyo baba yake wala mama yake na anapoamua kuchukua uamuzi wa kumuacha wala haumiagi. “Yaani mimi kukaa
muda na mwanaume sipendagi kabisa na sina mzuka huo kweli. 


Ndiyo maana mtu nikiamua kumbwaga anahaha na wengine watabembeleza weee lakini wala sina tabia ya kurudi nyuma, kwa kifupi sipendi kudumu na mpenzi,” alisema Uwoya
aliyewahi kuwa kwenye uhusiano na wanaume mbalimbali kabla ya kuolewa na msakata kabumbu raia wa Rwanda,  Hamad Ndikumana ambapo ndoa yao haikudumu.

No comments