• Latest News

  July 31, 2016

  Victoria Kimani amweka wazi mpenzi wake

  Muimbaji wa Kenya anayefanya kazi zake nchini Nigeria, Victoria Kimani kwa mara ya kwanza amemweka wazi mpenzi wake.

  Ni muda mrefu muimbaji huyo amekuwa akimficha mpenzi wake na huku akionekana kuwa karibu na mchezaji wa soka wa ligi ya Uingereza, Victor Wanyama hali iliyozua maswali kwa mashabiki kuwa wawili hao wana mahusiano lakini muimbaji huyo aliipinga kauli hiyo.
  Alhamis ya wiki hii muimbaji huyo alitimiza miaka 32 na alitumia nafasi hiyo kupiga picha na kumtambulisha mpenzi wake huyo kwa mashabiki wake kupitia mtandao wa Snapchat na kuandika, “Me and my baby.”
  “I Couldn’t be more grateful for you @iam_sos1 You have a Heart of Gold ❤️.” aliandika post hii kwenye picha nyingine aliyoiweka kwenye akaunti yake ya instagram.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Victoria Kimani amweka wazi mpenzi wake Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top