Header Ads

Wateja wa Vodacom Kujichagulia Vifurushi Wavitakavyo #YaKwako2

Katika dhamira yake ya kufanya ubunifu wa teknolojia kwa ajili ya kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa kuwapatia huduma bora za kurahisisha maisha na kwa gharama nafuu leo kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua ofa mpya maalum kwa wateja wake inayojulikana kama “Ya kwako tu” itakayowawezesha kujipatia vifurushi vya gharama nafuu kwa kadri ya matakwa yao wapendayo kuanzia vya huduma ya kuperuzi intaneti (Mitandao ya kijamii, Youtube, Whatsapp na kadhalika),kupiga simu (Kuenda mitandao yote) na kutuma ujumbe mfupi wa maneno.
Ili kupata huduma ya ofa hii ya“Ya kwako tu” mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga simu namba*149* 03# kupata orodha ya huduma anayohitaji kutumia.

  voda 2
Mkurugenzi wa mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) akifafanua jambo wakati wa Uzinduzi ya huduma mpya ya ”Ya kwako tu” itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujipatia vifurushi vya gharama nafuu kadri ya matakwa yao wapendayo kuanzia vya huduma ya data,kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno. Ili mteja aweze kujiunga na huduma hii anatakiwa kupiga namba*149* 03# na kuchagua ofa ya kwako tu, anayeshuhudia kushoto ni Afisa Mkuu wa Idara ya masoko wa kampuni hiyo, Ashutosh Tiwary na Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa kampuni hiyo, Danilo De Sousa.
voda 3

Waandishi wa habari wakiwa kazini.

No comments