Header Ads

Wema amfyatua Zari ni baada ya Zari kumchokonoa kisa mtoto!Ametibuka tena! Siku chache baada ya kutangaza kuwa hana kinyongo na anataka kukutana na mwandani wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anadaiwa kumfyatua mwanamama huyo kisa kikiwa ni suala la kumchokonoa ishu ya kupata mtoto. Katika maelezo yake, wiki mbili zilizopita, Wema alilieleza gazeti pacha la hili, Ijumaa kuwa, hajawahi kumchukia Zari wala kufikiria kumchukulia bwana’ke ila baadhi ya wapambe wake wamekuwa wakichochea kuwepo kwa tofauti kati yao hivyo akaomba kukutanishwa na mwanamama huyo. 

ZARI AMCHUKULIA VIBAYA 
Alichokifanya Wema anayedaiwa kurudiana na Diamond ilikuwa ni kumwambia Zari anatakiwa kuwa na amani na
familia yake, wala asisikilize maneno ya watu kwa sababu hawezi kumuingilia kwenye uhusiano wake lakini inadaiwa mwandani huyo wa Diamond alimchukulia vibaya. Habari kutoka makundi yanayojiita Wema Daily na Team Wema zinadai kuwa, tofauti na matarajio yao kuwa Zari angetoa sapoti kwa kuwa Wema alimzungumzia vizuri (positive), walishtushwa kusikia kuwa kwa upande wake amerusha dongo. 

 
POVU LA SNAPCHAT 
Mara baada ya Wema kufunguka, inadaiwa kwamba, hivi karibuni Zari alitupia video kwenye Mtandao wa Kijamii wa Snapchat (mtandao maalum kwa video na picha), akionekana kukasirishwa na kitendo cha kupambanisha na wanawake ambao hawajaingia ‘leba’ kujifungua. Zari anadaiwa kuitupia video hiyo kwenye Snapchat badala ya Instagram kwa sababu kwenye mtandao huo, mastaa wapo huru ‘kutoa povu’ kwa kujiachia kwa kirefu zaidi ambapo alisema: “Na wengine acheni kunifananisha na…(tusi) ambao hawajawahi kwenda leba. “Mtoto mmoja tu leba wataonekana kama tikiti maji lililopasuliwa. Acheni! “Nikiwa na umri wa miaka 35 nina watoto wanne, bado mimi ni mrembo mno kunifananisha...”

 TAFSIRI KUTOKA TEAM WEMA 
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa Wema,
maneno hayo ya Zari yalifikishwa kwa mlimbwende huyo
akiambiwa kwamba alilengwa yeye kwani hakuna staa mwingine Bongo ambaye amekuwa akipambanishwa naye hasa linapokuja suala la mtoto. “Unajua mwanzoni Tema Wema walipokuwa wakimwambia Wema kuwa Zari amemtusi na kumkejeli juu ya suala la kupata mtoto, hakutilia maanani hadi alipotafsiriwa vizuri kuwa ni yeye aliyesemwa na Zari. “Sasa hapo ndiyo Madam akawaka vibaya maana alipoulizwa anadhani Zari amemaanisha nani zaidi yake, alikosa jibu. Unaambiwa hapo ndipo alipoanza kuwajibu kuwa wamwambie Zari kuwa yeye siyo Mungu anayepanga wa kumpa mtu mtoto na wa kumnyima.

 ZARI ANAMKUFURU MUNGU?
 “Anasema kama amejaliwa watoto wanne angenyamaza kwani Mungu akiamua anaweza kumnyang’anya wote hivyo aache kumkufuru Mungu. “Kwa kweli Madam anaamini rungu ambalo Mungu atampiga Zari hatalisahau milele. Unajua Wema aliposema kuwa hana kinyongo na Zari alimaanisha maana mimi namjua vizuri. “Ni watu wangapi walishamkosea Wema na akawasamehe? Kwani ilikuwaje kwa Kajala Masanja au Snura Mushi? Ninavyomjua akisema hana kinyongo ni kweli hana kinyongo hivyo kama kweli Zari alimlenga yeye, amuombe msamaha,” kilisema chanzo hicho. 
HUYU HAPA WEMA 
Baada ya kusikiliza kinachosemwa juu ya sakata hilo Wikienda lilimtafuta Wema, alipopatikana aligoma kumzungumzia Zari kwa kina kwa maelezo kuwa yupo kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. “Sina muda wa kubishana na mtu, ninachojua ipo siku nitatinga leba na kuitwa mama,” alisema Wema kwa kifupi akisisitiza kuwa yupo kwenye mfungo.

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA/GPL

No comments