Header Ads

Wema, Kajala na Wolper wafumuliwa kisa tabia ya kugombea mabwana!

KUTOKANA na mastaa wengi wa kike kuwa na tabia ya kugombea mabwana na kuwabadilisha kila kukicha, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Jimmy Mafufu ameibuka na kuwafumua, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili. 
 
Licha ya kutowataja majina moja kwa moja Wolper, Wema na Kajala, Mafufu aliwachana kwa ujumla waigizaji wote ambao wana skendo hizo chafu hususan walizonazo warembo hao ambao wamesharipotiwa kwa nyakati tofauti kuibiana mabwana. Akipiga stori na mapaparazi wetu kwenye mahojiano maalumu, Mafufu alisema  kutokana na tabia ya uchangudoa kuzidi kukithiri kwenye tasnia ya filamu na kusababisha kuporomoka na kuichafua, kwa sasa wako kwenye maandalizi ya sheria maalum ya chama hicho ambayo itawaondoa wote waliovamia fani hiyo.


“Wasanii wengi wa kike wamevamia fani, wengine waliletwa na wapenzi wao ndiyo maana hawaumizwi kabisa na kuporomoka kwa tasnia ya filamu, wamefanya ni sehemu ya kuuza sura zao kwani mapedeshee wa mjini wanawataka sana watu maarufu. “Wasanii wa kike wa mikoani wanatia aibu, wanaona kuwa na skendo ndiyo umaarufu, wamesha-athiriwa na maisha wanayoyaona ya mitandaoni ya kina Wema, Wolper, Kajala na Uwoya na kuona kwamba ndiyo halisi kumbe nao wana upande wa pili, tunaendelea kuzalisha vyangudoa kila kukicha hivyo hatuko tayari kuona tasnia hii ikifa, ndiyo maana kuanzia mwezi huu wa saba tunatunga sheria za kuwaondoa wasiofaa. “Tutakaowaondoa ni wale wenye tabia za kugombea mabwana, kuvaa nusu utupu na wanaobadili mabwana kila kukicha kwa ajili ya kutafuta kiki, wale ambao wamepitia kwenye
vikundi wengi wao hawana matatizo, maana sijawahi kusikia Riyama au Monalisa wamegombea mabwana kwa sababu wanajitambua na wanajua maadili ya sanaa,” alisema Mafufu. Aidha, aliendelea kusema mastaa wa kike wengi kwa sasa wamekuwa wakijiona wao ni keki, kwani wapo wasanii chipukizi wanaowaomba wawachezeshe kwenye filamu zao kwa malipo mazuri tu ya hadi milioni mbili, lakini wanawakatalia au wanachukua hela na kutokomea kwa sababu wanajua mabwana walionao wakiwafuata walipo na kuwabusu tu wanapata dola elfu kumi. 

 
 Kajala Masanja.

“Tunataka tutokomeze tabia ya kuokotaokota watu mitaani na kuwaingiza kwenye filamu maana hao ndiyo wanaotuharibia fani na ugomvi wowote wa wasanii wa kike Bongo Muvi huwa unatokana na kunyang’anyana mabwana tabia ambayo siyo nzuri kwani inaleta doa ndani ya tasnia,” alisema Mafufu. 
 
KUMBUKUMBU Wema na Kajala waliwahi kuingia kwenye mgogoro kutokana na Kajala kumchukua mwanaume aliyekuwa mpenzi wa Wema aliyejulikana kwa jina la CK huku pia Wolper akiingia kwenye bifu kali na Husna Maulid wakimgomba.

CHANZO: RISASI JUMAMOSI

No comments