Header Ads

Yanga na Azam kuendelea kupangua ratiba ya ligi


Baada ya kupokea lawama nyingi msimu uliopita kutokana na mabadiliko ya ratiba ya ligi, Shirikisho la soka Tanzania TFF, limetoa tahadhari kabisa kwa usumbufu huo kuweza kutokea tena kwa ligi ijayo.Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi
Rais wa shirikisho la soka nchini TFF, Jamal Emil Malinzi, amesema kuna uwezekano mkubwa wa mabadiliko ya ratiba ya ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2016-17, yakafanyika kutokana na ushiriki wa klabu za Young Africans pamoja na Azam FC katika michuano ya kimataifa, ambapo mfumo wa usafiri ni changamoto kubwa Africa.
Malinzi amesema mabadiliko hayo huenda yakafanyika kati kati ya msimu, kutokana na Jiografia ya bara la Afrika, ambayo inazinyima nafasi klabu shiriki kwenda nje ya nchi kucheza michezo yao kimataifa na kurudi mapema nchini.
Amesema suala hilo linapaswa kuwa wazi kabla ya kutoka kwa ratiba ya ligi kuu ili kuondoa malalamiko ambayo kwa msimu uliopita yalionekana kupewa nafasi kubwa miongoni mwa wadau wa soka nchini, huku TFF ikiwa mstari wa mbele kubebeshwa lawama.

No comments