Header Ads

Amber Lulu Atamani Kujenga Bar Chumbani Kwake!

amber lulu (1)
Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ akiwa nyumbani kwake.
Msomaji wa Mpaka Home, leo tunaye mwanadada ambaye hivi sasa ndiyo habari ya mjini kwenye mitandao ya kijamii, huyu si mwingine ni Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ anayeishi Mwananyamala jijini Dar na ndugu yake aitwaye Bhoke au Kibonge Sexy. Ungana nami kujua mambo mengi kuhusu mrembo huyu.
amber lulu (5)Mpaka Home: Mambo vipi Lulu? Ni ajabu leo nimekuona umevaa dera?
amber lulu (3)Lulu: Hahahaa! Mbona kawaida tu nikiwa ‘kihome home.’
amber lulu (6)Mpaka Home: Sawa, tukiachana na dera lakini watu wengi wanakuchukulia tofauti na mavazi yako ya vichupi, wewe unalizungumziaje hilo?
amber lulu (7)Lulu:  Unajua katika maisha kila mtu anamtazamo wake, unaweza ukavaa dera au baibui na watu bado wakakusema vilevile. So mi sioni tatizo ilimradi najifahamu niko vizuri kitabia.
amber lulu (4)Mpaka Home: Vipi kwenye upande wa familia, yaani wazazi wako nao wanaona sawa tu unavyovaa?
amber lulu (8)Lulu: Mwanzoni ndiyo palikuwa hapatoshi lakini sasa hivi wanaelewa vile vichupi ni kazi na si kitu kingine.
Mpaka Home: Oke, vipi unapokuwa hapa nyumbani unapenda kufanya nini?
amber lulu (9)Lulu: Kufanya usafi mtu wangu, si unajua mwanamke mazingira!
Mpaka Home: Unaonekana ni mtu wa viwanja sana, unaweza kukaa jikoni na kupika kweli?
amber lulu (10)Lulu: Mbona napika jamani! Tena huwa napenda kula chakula nilichopika mwenyewe.
Mpaka Home:  Unapendelea kupika chakula gani hasa?
amber lulu (11)Lulu: Pilau ndiyo best kwangu! Niko vizuri sana hata kwenye kuipika.
amber lulu (2)Mpaka Home: Hivi unaweza kumaliza siku mbili bila kwenda kujirusha?
amber lulu (12)Lulu: ‘Sometimes’ hata mwezi, mimi mbona siyo mtu wa viwanja kiivyo!
Mpaka Home:  Nini ambacho unatamani kiwepo hapa nyumbani kwako na hakipo?
amber lulu (13)Lulu: Natamani kuwepo na baa ndogo ya ndani, nitainjoi sana.
Mpaka Home: Vipi una mchumba na kama unaye anaongeleaje mavazi yako?
Lulu: Nilikuwa naye zamani sasa hivi nipo singo, lakini hata yeye alikuwa haelewagi mavazi yangu mwanzo lakini baadaye alielewa.

No comments