Header Ads

BABA’KE KAJALA ASHIKILIWA NA PLISI JIJINI DAR KISA KIPO HAPA!


Baba wa staa wa fi lamu za Kibongo, Kajala Masanja, mzee Paul Masanja anadaiwa kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini hapa tuhuma zikiwa ni kujipatia shilingi milioni kumi na laki tano (10,500,000) kutoka kwa mfanyabiashara mmoja kwa nia inayodhaniwa kuwa si nzuri. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kipolisi, mzee huyo ambaye ni askari mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania aliingia matatani baada ya mfanyabiashara huyo kufi ka kituoni hapo kumlalamikia. 

“Jamani baba’ke Kajala yule msanii, anashikiliwa Oysterbay tangu Jumapili. Anadaiwa kujipatia kiasi cha shilingi milioni kumi na nusu kwa njia isiyoeleweka kutoka kwa mfanyabiashara mmoja. “Nasikia alimfuata mfanyabiashara huyo na kumuomba kiasi hicho cha pesa kwa vile ameagizwa na mtu mmoja mkubwa serikalini na kwamba zingerudi baada ya muda,” chanzo kililiambia gazeti hili, Jumatatu iliyopita. K i k a e n d e l e a : “Kuna madai mazito kidogo kwani nasikia ametajwa hadi mkuu wa polisi kwenye ngazi ya juu kwamba eti alimtuma mzee huyo lakini nasikia hakutumwa ila ilikuwa njia ya yeye kujipatia kiasi hicho cha pesa.


” Madai yanazidi k u m i m i n i k a kwamba, tangu mzee huyo ashikiliwe kituoni hapo Jumapili, ndugu wamekuwa wakihaha kumtoa lakini imekuwa vigumu kutokana na polisi kuwa kazini kuchunguza ukweli wa madai hayo. Juzi, Amani lilimsaka Kajala kwa njia ya simu ili kumsikia anasemaje kuhusu madai hayo ambapo alisema: “Baba hakumtapeli yule mfanyabiashara, ila walikopeshana wenyewe huko. Sasa ili azipate pesa zake ndiyo maana akatumia njia ya kusema amemtapeli lakini ukweli hakuna utapeli.

” Juzi, Amani lilimpigia simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzana Kaganda kwa lengo la kutaka kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa madai ya mzee huyo, ambapo alithibitisha kukamatwa kwa mzee huyo na kuongeza kwamba ameachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi dhidi yake ukiendelea.

No comments