Header Ads

Bosi wa redio Ammwaga Lulu, Apukutika mwili kwa stress, Adaiwa kuomba radhi getini!

Hii ndiyo habari ya mjini! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amedaiwa kuachwa solemba kwa kumwagwa na mchumba wake ambaye ni bosi wa redio moja maarufu Bongo (jina lipo) kwa madai ya kuwa na michepuko. 


NI YULE ALIYEMNADI MITANDAONI Kwa muda mrefu, Lulu alikuwa akijinadi kwa mbwembwe nyingi mitandaoni akimsifia mchumba wake huyo kwamba hawataachana hivyo kitendo cha kumwagwa, kimegeuka kuwa fedheha kubwa kwa mashabiki wake. 

ISHU ILIVYOBUMBULUKA Chanzo makini ambacho kipo karibu na familia ya muigizaji huyo mdogo ki-umri ila mkubwa kwa ‘majanga’, kilivujisha mchapo kuwa, Lulu amejikuta akitupiwa virago na bosi huyo wa redio baada ya kufuatilia njia zake na kubaini kuwa ana michepuko kitendo ambacho kilimkatisha tamaa. “Jamaa alimfanyia umafia kupitia simu yake. Alishikilia mawasiliano yake kwa kutumia teknolojia na akagundua Lulu anawasiliana na wanaume wengine. 


AMPIGA CHINI “Baada ya kukusanya ushahidi wa kutosha, jamaa (bosi wa redio) hakuwa na mswalia Mtume, alichokifanya ni kumtimua nyumbani kwake sababu aliona hana sifa ya kuwa mke,” kilidai chanzo hicho. 
KUMBE ILIKUWA AMUOE Chanzo hicho makini kilizidi kutiririsha ubuyu huo wa uhakika kwa kudai kuwa, bosi huyo alishafikia hatua
ya kuanza taratibu za awali za kuelekea kwenye ndoa lakini akaghairi kwa kuona mtoto wa kike huyo amepoteza sifa. “Huwezi amini, yaani (amtaja jina bosi wa redio) alikuwa amuoe kabisa. Kila kitu kilikuwa kwenye mstari, ilikuwa ni muda mchache sana vikao vianze na tarehe rasmi ya ndoa itangazwe lakini ndiyo hivyo tena kimenuka,” kilidai chanzo hicho. 

AMWAGA MACHOZI GETINI Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, kufuatia ‘kibuti’ hicho, Lulu alilazimika kwenda kuomba ‘hisani’ kwa mchumba wake huyo ili arudishe moyo nyuma lakini aliambulia patupu kwani jamaa alishasema hayupo tayari kurejea ‘Misri’ wakati yupo Kanani. “Kabubujika machozi kwelikweli pale getini, jamaa hakumfungulia, yaani mtoto wa kike alilia hatari lakini wapi,” kilidai chanzo hicho. 
AJITOA INSTAGRAM Chanzo hicho kilidai kuwa, baada ya kuona mambo magumu na hakuna uwezekano wa kupata msamaha, Lulu alijitoa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kukwepa ‘maneno maneno’. 
APUKUTIKA MWILI Kutokana na bomu hilo alilopigwa, chanzo hicho kilidai kuwa binti huyo alijikuta taratibu akikonda kwa mawazo kwani licha ya kuiacha njia kuu, bosi huyo wa redio alikuwa ndiyo kila kitu katika maisha yake kwa kuwa alikuwa akimgharamia mahitaji yote ya kibinadamu. “Nyinyi fuatilieni, Lulu wa sasa si yule, kakonda kwelikweli, chezea kuachwa wewe. Mawazo yalimjaa japo kwa sasa kidogo ameanza kuzoeazoea mazingira ya kuachwa,” alisema mtoa ubuyu huyo.
IJUMAA LATHIBITISHA KUPUKUTIKA Katika pitapita zake, Ijumaa Wikienda lilimbamba Lulu katika sherehe ya Send off ya muigizaji Neema Chande kwenye Hoteli ya Giraffe, Mbezi Beach jijini Dar akiwa amekonda, alipoulizwa sababu alijitetea kuwa anafanya mazoezi. “Mimi nafanya mazoezi, watu unajua wanaongea mengi bila kujua lakini kupungua kwangu kumesababishwa na mazoezi,” alisikika Lulu. 

KUHUSU KUACHWA SASA Alipotafutwa na gazeti hili na kusomewa mashtaka hayo ya kuachika, Lulu kama kawaida yake, mdomo wake ulikosa staha, akaanza kuropomosha maneno bila mpangilio. “Wewe sikia, nimeshasema… sitaki mambo ya kijinga, usiniulize hizo habari. Wewe kwanza ni nani? Waambie hata hao mabosi zako, nishasema sitaki waniulize kitu, tena mniache kabisa,” alitiririka Lulu. 
MAMA’KE AJIKANA Jumamosi iliyopita, mwanahabari wetu alimvutia waya mama mzazi wa mwigizaji huyo, Lucresia Karugila kupitia namba yake ambayo anapatikana kila siku lakini siku hiyo, simu yake ilipopokelewa, sauti ya mwanamke ilisikika ikisema yeye si mama Lulu. “Utakuwa umekosea namba mimi si mama Lulu,” ilisikika sauti upande wa pili.
 HISTORIA YAKE Kabla ya kuwa na bosi huyo wa redio, Lulu aliwahi kuwa na uhusiano rasmi na marehemu Steven Kanumba kabla ya kunasa kwa jamaa mwingine ambaye naye waliachana huku akitajwa kutoka na baadhi ya mastaa Bongo lakini wote waliishia njiani bila kuingia kwenye ndoa. 

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA

No comments