• Latest News

  August 19, 2016

  Chuchu Hans akesha akiomba amzalie Ray

  MSANII mkali wa Bongo Muvi, Chuchu Hans amefunguka kuwa mara nyingi amekuwa akisali na kuomba ili aweze kufanikiwa kupata mtoto na mpenzi wake Vincent Kigosi ‘Ray’. 
   
  Akizungumza na gazeti hili, Chuchu alisema kuwa amekuwa akisikia minong’ono, baadhi wakihoji kwa nini hamzalii mpenzi wake huyo lakini ukweli ni kwamba siyo kwamba hataki bali Mungu bado hajapanga. 

  “Mimi nakesha nikiomba nipate mtoto, siyo kwamba nanasa kisha natoa au nambania mpenzi wangu, hapana! Natamani sana iwe hivyo lakini naona Mungu hajapanga ila kwa maombi ninayofanya naamini ipo siku ndoto yangu itatimia,” alisema Chuchu anayefanya vizuri kupitia Tamthiliya ya Usaliti
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Chuchu Hans akesha akiomba amzalie Ray Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top