Header Ads

DEAL DONE, PAUL POGBA PETE NA CHANDA NA MAN UNITED, ADA YA PAUNI MILIONI 100, MSHAHARA WA PAUNI 290,000 KWA WIKI


Paul Pogba ndani ya jezi ya Manchester United baada ya kukamilisha usajili wake akitokea Juventus.
21
Pogba katika jezi za Manchester United.
5
Pogba akielekea kwenye uwanja wa mazoezi wa Man United wa Carrington jana mchana kwa ajili ya vipimo.
7
Mama mzazi wa Pogba, Yeo Moriba naye akielekea kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United jana.
4
Pogba katika pozi na baadhi ya wafanyakazi wa Manchester United.
6
Pogba akiwasili kwa ndege akitokea Nice, Ufaransa baada ya kutoka kwenye mapumziko huko New York, Marekani.
8
Kaka wa Pogba, Mathias Pogba anayechezea Partick Thistle, akiondoka hotelini pamoja na mama yake.
9
Pogba akiaga mashabiki wakati akiondoka Manchester United mwaka 2012.
HATIMAYE Manchester United imekamilisha usajili wa Mfaransa Paul Pogba kutoka klabu ya Juventus ya Italia kwa kitita cha Pauni milioni 100 zaidi ya bilioni 284 za Tanzania.
Pogba atakuwa akilipwa Pauni 290,000 kwa wiki zaidi ya milioni 824 za Tanzania na amesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano pamoja na kipengele kinachomruhusu kuongeza mwaka mmoja.
Staa huyo mwenye miaka 23, amevunja rekodi ya usajili iliyokuwa inashikiliwa na mchezaji wa Real Madrid,  Gareth Bale aliyesajiliwa kwa Pauni milioni 86 zaidi ya bilioni 244 za Tanzania akitokea Tottenham kwenda Real Madrid.
Pogba aliondoka Manchester United mwaka 2012 kwa fidia ya Pauni 800,000 zaidi ya bilioni 2 za Tanzania baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
Staa huyo amesema Manchester United ndiyo klabu sahihi kwake kupata mafanikio anayoyahitaji na atakuwa akivaa jezi namba 6.
Kwa mshahara huo wa zaidi ya milioni 824 kwa wiki, Pogba atakuwa akilipwa zaidi ya bilioni 3 kwa mwezi na kwa mwaka atakuwa akikunja zaidi ya bilioni 39 za Kitanzania.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji 10 waliosajiliwa kwa dau kubwa;
Paul Pogba – Juventus kwenda Man United £100m
Gareth Bale – Tottenham kwenda Real Madrid £86m
Cristiano Ronaldo – Man United kwenda Real Madrid £80m
Gonzalo Higuain – Napoli kwenda Juventus £76m
Neymar – Santos kwenda Barcelona £72m
Luis Suarez – Liverpool kwenda Barcelona £63m
James Rodriguez – Monaco kwenda Real Madrid £60m
Angel di Maria – Real Madrid kwenda Man United £60m
Kaka – Milan kwenda Real Madrid £56m
Kevin De Bruyne – Wolfsburg kwenda Man City £55m

No comments