• Latest News

  August 02, 2016

  Diamond: Zari atajifungua mwezi Disemba mwaka huu mtoto wangu wa pili

  Mkali wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.
  Diamond

  Muimbaji huyo amesema yeye na mpenzi wake Zari wanategemea mtoto wa kiume.

  “Yah kweli mimi ni baba kijacho,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo Tena “Natarajia Mama Tiffa anipatie tena mtoto mwingine, atakuwa wa kiume,”

  Aliongeza, “Na itakuwa mwezi Disemba mwaka huu! Baada ya hapo sitaongeza tena mtoto mwingine, ni muda wa kula bata sasa ndio unafata na watoto wetu wawili”

  Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni atatimiza mwaka mmoja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Diamond: Zari atajifungua mwezi Disemba mwaka huu mtoto wangu wa pili Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top