Header Ads

Dimpoz afunguka penzi la Jokate Mwegelo ‘Jojo...wadaiwa kuwa wapenzi!

 

 Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Jojo’.

Mtandaoni kuliibuka uvumi kuwa mastaa wawili wa Bongo Fleva, Omar Faraj Nyembo ‘Dimpoz’ na Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ bila kujua, wanachanganywa penzini na mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Jojo’, Dimpoz ameibuka na kutoa ufafanuzi. Kwenye uvumi huo, Dimpoz anadaiwa kuwa alikuwa nyumbani kwake na Jokate na hata alipoulizwa na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio, bila kujitambulisha, awali alikiri kwamba kweli Jokate alikuwa kwake lakini kwa muda ule alitoka. 
 
 Dimpoz akiwa na Wema Sepetu.

Baadaye alipogundua anayezungumza naye ni mtangazaji, aliruka viunzi na kusema Jokate ni mshkaji wake ambaye wana uhusiano wa kawaida kikazi na kamwe hawezi kuwa naye kimapenzi. Mbali na Dimpoz, kwenye ‘klipu’ hiyo, anasikika pia mrembo Jokate akiomba apigiwe kesho kwani alikuwa kwenye eneo ambalo halina usikivu mzuri.
 


Akizungumzia suala hilo, Dimpoz alisema hana uhusiano na Jokate na hata hiyo klipu inayosikika akizungumza na mtangazaji huyo, si yake. “Mimi sina uhusiano na Jokate. Sijawahi kuzungumzia ishu yoyote inayomhusu Jokate hivi karibuni. Jojo namheshimu na yeye ananiheshimu pia, tungekuwa wapenzi wewe m w e n y e w e m w a n d i s h i ungejua. “Mimi sijajua hayo maneno yameibukia wapi na aliyeyaibua ni nani, si unajua tena haya mambo ya mitandao siku hizi,” alisema Dimpoz. Mwanahabari wetu alimvutia waya Jokate ili kumsikia kama ana lolote kuhusu taarifa hiyo, simu yake
iliita bila kupokelewa. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kuhusu ishu hiyo, bado hakujibu. Mbali na Jokate, Dimpoz aliwahi kudaiwa kutembea na Mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ ambapo zilizagaa picha zinazowaonesha wakiwa ‘klozi’ kitandani.

No comments