• Latest News

  August 02, 2016

  EXCLUSIVE: MO DEWJI KUMWAGA MAMILIONI NDANI YA KLABU YA SIMBA LEO  Kuna taarifa zilizotufikia punde zinaeleza bilionea kijana Mohammed Dewji, amekubali kuipa Simba fedha zitakazoisaidia kufanya usajili.


  Bado haijajulikana atatoa kitita cha kiasi gani lakini taarifa zinasema, Dewji maarufu kama Mo atatangaza kiasi atakachotoa leo.

  Jana, uongozi wa Simba ulimuandikia barua kumuomba Mo atoe fedha za usajili kama alivyoahidi kusaidia wakati akitangaza nia yake ya kutaka kununua asilimia 51 za klabu ya Simba.

  "Kuna uwezekano atatoa hadi zaidi ya Sh milioni 80, lakini hatujajua, ila taarifa zinasema Mo amekubali kutoa fedha hizo," kilieleza chanzo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: EXCLUSIVE: MO DEWJI KUMWAGA MAMILIONI NDANI YA KLABU YA SIMBA LEO Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top