• Latest News

  August 13, 2016

  EXCLUSIVE: NEEMA YANGA, FIFA YAFUNGUA DIRISHA LA USAJILI, NI KWA SAA 48 TU

  Kuna taarifa kwamba Shirikisho la Soka la Kimataifa limefungua tena dirisha la usajili kwa saa 48.

  Taarifa kutoka ndani ya TFF zinasema Kuanzia leo, dirisha hilo la usajili litafungwa Jumapili saa 6 usiku, kwenda Jumatatu na hii ni nafasi kwa klabu ambazo hazikuwasilisha usajili kukamilisha.

  Mabingwa wa Tanzania, Yanga pamoja na Coastal Union pia African Lyon zilikuwa kati ya timu za Ligi Kuu Bara na Daraja la Kwanza ambazo hazikuwa zimekamilisha usajili.

  Hii inaweza kuwa nafasi ya klabu hizo kumalizana na suala hilo ili kutulia na kulenga maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza Ligi Kuu Bara, wiki ijayo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: EXCLUSIVE: NEEMA YANGA, FIFA YAFUNGUA DIRISHA LA USAJILI, NI KWA SAA 48 TU Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top