• Latest News

  August 19, 2016

  EXCLUSIVE…KESSY RUKSA YANGA, TFF YASEMA NI MCHEZAJI HALALI WA YANGA

  Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji imepitisha usajili wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha jina la mchezaji Hassan Kessy kuichezea Young Africans. Hii ni kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas. 
      Kessy alikuwa katika mgogoto mzito kutokana na kile kilichodaiwa kusajiliwa na Yanga kabla hajamalizana na Simba, hali ambayo ilifanya Simba kukataa kutoa barua ya uthibitisho kuwa imemalizana na Kessy.  Kitendo cha Simba kutoandikiwa barua hiyo kimesababisha akose mechi za kimataifa licha ya kuwa katika kikosi cha Yanga kwa wiki kadhaa.

  Jumatano iliyopita alicheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC kitendo ambacho kililalamikiwa na baadhi ya wadau wa Simba na Azam ambao walidai kuwa inakuwaje TFF inamruhusu kucheza wakati usajili wake haujakamilika.

  Kuruhusiwa kwa Kessy sasa kutamfanya mchezji huyo kuwa huru kuitumikia Yanga katika msimu mpya wa 2016/17 unaotarajiwa kuanza wikiendi hii.


  Habari ya Kessy kuruhusiwa kuichezea Yanga ni neema kubwa kwa kocha wake, Hans van Pluijm ambaye amekuwa akihitaji huduma yake lakini alikuw akiikosa kutokana na mgogoro huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: EXCLUSIVE…KESSY RUKSA YANGA, TFF YASEMA NI MCHEZAJI HALALI WA YANGA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top