Header Ads

FLORA MBASHA, EMMANUEL MBASHA WAIBUA MAPYA KISA MAJINA

 
Waimbaji nyota wa Injili nchini, Emmanuel Mbasha na aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha, wameibua mpya baada ya wawili hao kuoneshana umwamba wa matumizi ya majina yao kwa sasa. Awali, Mbasha aliliambia Risasi Mchanganyiko kuwa hataki kusikia aliyekuwa mkewe, Flora akitumia jina la Mbasha, kwani maisha yao yameshathibitisha kuwa hivi sasa kila mtu na maisha yake. “Kwa sasa kila mtu ana maisha yake, namtaka Flora aache mara moja kuendelea kutumia jina langu, maana naona hata kwenye mitandao ya kijamii anaendelea kulitumia pia kwenye shughuli zake mbalimbali, namshangaa maana kama ni ndoa ilishavunjika na hatuko pamoja tena, inakuwaje anatumia jina langu, aache mara moja kwa kweli sitaki
alitumie,” alisema Mbasha. Risasi Mchanganyiko lilipomtafuta Flora na kumweleza juu ya madai ya Mbasha, alisema yeye hivi sasa anatumia jina la Madam Flora. “Jina la Flora halijabadilika, lililoongezeka ni Madam tu, baada ya kupitia changamoto mbalimbali ambazo nisingependa kuzizungumzia katika maisha na safari yangu kihuduma, nauhesabu wakati huu kama mwanzo mpya, nikaona ni vema nitumie
Madam Flora, kila jambo na wakati wake,” alisema katika ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi. Katika kusisitiza, Flora alituma sehemu ya akaunti yake katika mtandao wa kijamii, ikionesha kuwa jina analolitumia ni Flora Henry na katika mabano akiandika Madam Flora. Ndoa ya wawili hao ilipata mpasuko mkubwa baada ya kutokea
kutokuelewana, kulikosababisha Mbasha kufunguliwa kesi ya kudaiwa kumbaka shemeji yake ambayo hata hivyo, mahakama ilikosa ushahidi wa kumtia hatiani.

No comments