• Latest News

  August 11, 2016

  HAPA NDIPO LILIPOFIKIA SAKATA LA MAVUGO, SIMBA NA VITAL'O....  Pamoja na klabu ya Simba kusisitiza mshambuliaji wake mpya, Laudit Mavugo ni mali yake, Vital’O ya Burundi, imeendelea kusisitiza inammiliki.

  Vital’O imetuma nina lake kwenye Shirikisho la Soka la Burundi (BF) ikiwa ni sehemu ya wachezaji itakaowatumia msimu uliopita.

  Hali hiyo inaashiria mgogoro wa usajili kwa Mavugo ambaye amejiunga na Simba msimu huu akielezwa kumaliza mkataba na timu yake hiyo ya zamani.

  Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema, Mavugo hana tatizo lolote la usajili: “Ni mchezaji wa Simba na hakuna maelezo mengine zaidi.”

  MAVUGO
  Lakini Rais wa Vital’O, Benjamin Bikorimana amesema, Mavugo hajamaliza mkataba na timu yake kama inavyoelezwa.


  “Ni kitu cha kushangaza sana, Simba wanapoteza muda. ITC yake ipo kwetu, huyu ni mchezaji wetu na tuna mkataba naye, wanajisumbua,” alisema Bikorimana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HAPA NDIPO LILIPOFIKIA SAKATA LA MAVUGO, SIMBA NA VITAL'O.... Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top