• Latest News

  August 01, 2016

  HATIMAYE MO AIKABIDHI BARUA YAKE KWENYE OFISI YA EVANS AVEVA


  Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema tayari ameandika barua kwa uongozi wa Simba kueleza kuhusiana na uamuzi wake wa kutaka kununua hisa za Simba kwa asilimia 51.

  Mo amesema ameandika barua hiyo leo asubuhi baada ya kusikia baadhi ya viongozi wa Simba wakisema hakuwa amefanya hivyo.

  "Kweli hatukuwa tumeandika barua kwa kuwa nilitaka mchakato uchukue hatua. Baada ya hapo lingefuata suala labarua, lakini kwa kuwa wanasema lazima barua, basi acha tufanye hivyo.

  "Tayari barua imeandikwa na imepelekwa kwenye klabu, kukawa hakuna mtu na sasa imepelekwa ofisini kwa Aveva," alisema Mo.

  "Nilichoeleza kwenye barua yangu ni kilekile kwamba ninatoa ofa ya Sh bilioni 20 ili kupata hisa asilimia 51. Niko tayari kushirikiana na uongozi wakati wa mchakati kama ambavyo nilieleza awali," alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HATIMAYE MO AIKABIDHI BARUA YAKE KWENYE OFISI YA EVANS AVEVA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top