Header Ads

HATIMAYE, UONGOZI SIMBA WAOMBA MCHANGO WA USAJILI KWA MO DEWJIBARUA KUTOKA UONGOZI WA SIMBA KWENDA KWA MO DEWJI.
Sasa inaonekana mambo yanaanza kwenda vizuri na muunganiko wa umoja kati ya uongozi wa klabu ya Simba na Bilionea, Mohammed Dewji ambaye ni shabiki na mwanachama wa Simba, unaanza kukolea.

Hii ni baada ya leo, uongozi wa Simba kumkaribisha kwenye kikao cha kamati ya utendaji lakini baadaye umeandika barua pia kuomba fedha kwa ajili ya usajili.


Ombi hilo ni sehemu ya kumkumbusha Mo kutokana na ahadi yake kuwa yuko tayari kuchangia usajili.

Tayari Mo ametangaza nia yake ya kununua hisa asilimia 50 za klabu ya Simba kwa kutoa Sh bilioni 20.

No comments