• Latest News

  August 15, 2016

  HII NDIYO TAARIFA INAYOZAGAA MITANDAONI KUHUSIANA NA YUSUF MANJI KUACHIA NGAZI YANGA


  MANJI (KUSHOTO) AKIWA NA MAKAMU MWENYEKITI WA YANGA, CLEMENT SANGA.

  Habari za uhakika ambazo tumezipata kutoka katika chanzo cha uhakika ndani ya Yanga zinaonyesha kuwa mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf manji ameamua kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa yanga pamoja na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya Yanga na nembo yake .

  Hili ni anguko kuu kwa yanga endapo Bw Yusuf manji atajionda Yanga kutokana na ukweli kuwa tayari mahasimu wao wa jadi Simba wanakamilisha taratibu za kumkabidhi timu Bw mohamed Dewji MO.

  Uamuzi wa manji kujiondoa yanga unatajwa kuchangiwa na shutuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali, na wengine kutoka ndani ya yanga ambao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi na sio ya yanga.

  Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake .


  Hata hivyo viongozi wa Secretary ya yanga siku nzima ya leo wameonekana kuchanganyikiwa uku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka quality plaza zilizopo ofisi za Bw manji hatua inayoashiri kuna jambo kubwa linatokea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HII NDIYO TAARIFA INAYOZAGAA MITANDAONI KUHUSIANA NA YUSUF MANJI KUACHIA NGAZI YANGA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top