Header Ads

Hukumu Kesi Ya Babu Tale Bofya Hapa!

ILE kesi inayomkabili Meneja wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale ya kusambaza na kuuza DVD za mawaidha ya Shehe Hamis Mbonde bila ridhaa yake imeahirishwa tena na Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam hadi Agosti 24, mwaka ambapo hukumu itatolewa.
Akizungumza mbele ya mawakili na wahusika wa pande zote mbili leo asubuhi, Msajili wa Mahakama, Kayonza alianza kwa kutupilia mbali hoja ya mawakili wa upande wa Babu Tale, Robert Mkoba na Augustino Aluta iliyoomba kupewa muda zaidi kwa sababu ya mmoja kati ya mawakili wao (Paul Mgaya) ana udhuru na kwamba yupo jijini Arusha kwa semina.
“Mawakili mnaosikiliza kesi hii kwa upande wa Tale mpo watano, siwezi kuruhusu tena kuahirishwa kwa kesi hii kisa mmoja hayupo. Agosti 24 itakuwa siku ya hukumu na kutekelezwa ambacho kipo na niwaombe wote muwepo,” alisema Kayonza.
Awali kesi hiyo ilitakiwa itolewe hukumu Agosti 1 lakini kutokana na Mgaya kuumwa ilibidi kuahirishwa hadi leo (Agosti 10).
Wakili wa Shehe Mbonde, Mwesiga Muhingo akitolea ufafanuzi kuahirishwa kwa kesi hiyo alisema, siku hiyo ya hukumu iliyotolewa na msajili ni kuhusu kutekeleza yale ambayo mahakama iliagiza ambayo ni Tale kumlipa mteja wao (Shehe Mbonde) Sh. milioni 250 ama kwenda jela.
Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

No comments