Header Ads

HUYU COSTA NAYE WAKATI MWINGINE KAMA 'MWEHU', CHEKI HII


Pamoja na kwamba Diego Coasta aliisaidia Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England, msimu huu, lakini wakati mwingine anakuwa kama mwendawazimu.

Costa raia wa Hispania anapenda ubabe hata sehemu yenye utulivu au ambako hakuna sababu ya ubabe.

Mfano katika mechi hiyo waliyoshinda, alimkanya kipa wa West Ham United, Adrian nusura amvunje mguu.

Mazingira, hayakuwa yakionyesha kwamba alivyokwenda lazima angefanya hivyo. Lakini alionekana kulenga kwa makusudi kabisa kumuumiza.

Hata kama ndiyo ametokea Brazil Uswahilini, braza huyu naye kazini. Eeh!


No comments