Header Ads

Jennifer Lopez ampiga chini mpenzi wake ‘dogodogo’ Casper Smart

Jennifer Lopez (47) na Casper Smart (29) wameachana rasmi.

Wawili hao walianza mahusiano kuanzia Octoba 2011 kabla ya mwaka 2013 kuvunjika kwa mahuaiano hayo huku kila mmoja akiishi kivyake lakini baada ya muda mfupi walirudiana na kuishi pamoja.
Chanzo cha karibu cha mrembo huyo wa Pop kimedai kuwa J Lo amekuwa akiishi maisha yasiyokuwa na furaha ndani ya mahusiano hayo.
J Lo
Wikiendi iliyopita wawili hao walionekana wakiwa pamoja na wenye furaha kwenye nyumba ya Marc Anthony ambaye ni mzazi mwenzake na J Lo na walipiga picha ya pamoja.
Mwaka 2016 umeonekana kuwa wa balaa kwa mastaa wa Marekani kutokana na kuvunjika kwa mahusiano ya mastaa kadhaa akiwemo Iggy na Nick Young, Diddy na Cassie, Jason Derulo na Daphne Joy, na wengine wengi.

No comments