Header Ads

JOSE MOURINHO ASEMA AMEMALIZA USAJILI MANCHESTER UNITED

Mourinho takes Manchester United to Hull on Saturday, with both sides on six points

JOSE MOURINHO amewapa ushujaa wachezaji wake na kuwaambia uwezo wao unatosha kabisa kuipa Manchester United taji la Premier Legaue. 

Kocha huyo wa United anakipeleka kikosi chake kuvaana na Hull City Jumamosi hii katika mchezo wao wa tatu wa Premier League baada ya kushinda mechi mbili za mwanzo dhidi ya Bournemouth na Southampton.

 Katika mkutano wake na wachezaji kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United - Carrington, Mourinho akawaambia Wayne Rooney, Zlatan Ibrahimovic na wenzake kuwa hawahitaji  kusajili tena majina makubwa kiangazi hiki kwa kuwao waliopo wanatosha kuleta mataji Old Trafford.

No comments