Header Ads

Kajala Atangaza kusaka Mchumba mchumba mpya baada ya kuwa mpweke

MWIGIZAJI anayetamba na sinema ya Sikitu, Kajala Masanja, amefunguka kwamba kwa sasa anatafuta mchumba mpya baada ya kuwa mpweke kwa muda mrefu.
 
Msanii huyo alifunguka hayo baada ya paparazi wetu kumbana kuhusu habari zilizosambaa mtandaoni kuwa anatoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Msami Giovani ‘Msami Baby’ anayetamba na nyimbo za Mabawa na Yala Yala. “Msami ni mshikaji wangu tu, wala sina uhusiano naye wa kimapenzi, kwa sasa niko single (hana mchumba) natafuta mchumba mwenye sifa na vigezo aniondoe upweke, nahitaji mtu wa kuniliwaza na awe karibu nami muda mwingi.

“Kama angekuwa mchumba wangu lazima ningewaambia, na mchumba mpya nikimpata nitawaonesha ili mashabiki wangu wamjue shemeji yao mpya, sichagui rangi wala kabila. Mwanaume ninaye mhitaji lazima akidhi vigezo ninavyovihitaji kama mwanamke,” alisema Kajala. Mrembo huyo kwa sasa yuko jijini Lusaka nchini Zambia kushiriki filamu mpya ya Kwacha aliyoshirikishwa na waigizaji wa nchini humo ikiwa ni filamu yake ya kwanza kuigiza nje ya nchi tangu aingie kwenye fani ya uigizaji.

No comments