Header Ads

Kajala: Kama si mazoezi, ningekuwa nimekufa


 Msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja akifanya mazoezi.
MSANII wa filamu Bongo, Kajala Masanja ameanika siri ya kufanya mazoezi kila siku akiweka wazi kuwa, hilo limekuja kufuatia ushauri aliopewa na daktari wake aliyekuwa akimtibu tatizo la moyo. Akizungumza na Ijumaa kuhusu afya yake kwa sasa, Kajala alisema kuwa, watu wengi hawajui kilicho nyuma ya mazoezi anayofanya sasa lakini ukweli ni kwamba anafanya

hivyo kutokana na tatizo la moyo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu. “Kweli nafanya sana mazoezi lakini hii inatokana na ushauri wa daktari wangu kutokana na tatizo la moyo nililonalo. Kama siyo kufanya hivi yawezekana kabisa ningekuwa nimeshakufa zamani kama siyo kupata matatizo makubwa'' alisema Kajala.

No comments