Header Ads

Kanga Moja Kiunoni... MBENGEMBEGE - 20

 ILIPOISHIA: Akiwa ndani ya kanga moja na taulo kwa juu yake, mama Mei alitoka uani ambako alikutana na mzee mwenye nyumba, Hewa na mpangaji mwingine wakiwa wanazungumzia tukio la usiku, la mwizi kutimuliwa nyumba ya pili... SASA JIACHIE MWENYEWE.
 
HA! Kweli jamani?” aliuliza Mfaume aliyekuwa pembeni yao, maana yeye alikuwa ‘amepoteza fahamu’ baada ya kumaliza kazi na mama Mei. Mama Mei aliwasalimia huku akiwa mwenye aibu kubwa. Hata walipomsalimia, hakuwa mchangamfu. Maana hapo tayari, Mfaume anamfahamu kwa undani, mzee mweny
nyumba pia... “Hujambo binti?” mzee mwenye nyumba alimsalimia... “Sijambo, shikamoo...” “Marhaba! Halafu usiku wa kuamkia leo nimegonga sana kwako, baadaye nikagundua hata funguo haipo ndani ya mlango, ulifungua ukatoka. Ikabidi nilale sebuleni kwangu kusikiliza labda umepata matatizo, nikakusikia asubuhi ukiingia, ulikuwa wapi?” aliuliza mzee Hewa bila kujali mazingira. Mama Mei alijiumauma kwa sana maana anajua muda huo alikuwa kwa Mfaume, sasa yeye ajibu nini na pale walikuwepo Mfaume na yeye mzee Hewa... “Mh! Labda sikusikia, mimi nikishafunga mlango nina tabia ya kuchomoa funguo naiweka mahali, kwani haitakiwi?” alijibu mama Mei na kuongeza na swali juu... “Ha! Mbaya sana binti... mbaya! Mtu akija na funguo yake malaya anaingiza, anafungua na kuingia ndani na wewe upo... “Faida za kuacha funguo kwenye mlango ni kwamba, atakayetaka kuingiza funguo zake zitakwama maana
kutakuwa na funguo nyingine ndani.” “Ahaa! Basi nimejifunza,” alisema mama Mei huku akimwangalia Mfaume kwa macho ya kujiibaiba. Mama Mei alipitiliza hadi chooni, alipotoka alirudi ndani kwake na kukaa kitandani akijutia kwa kuwaza... “Yaani mimi ni mwanamke wa aina gani? Wanaume watatu kwenye nyumba moja wote nimelala nao, maana yake nini sasa? “Hivi nikiitwa maharage ya Mbeya au jamvi la wageni watakuwa wanakosea?” Mama Mei aliumia sana moyoni, lakini ilishatokea, akawa hana namna. Pia, kilichomuumiza kingine ni kubaini kuwa, kuachana na watu hao itakuwa ngumu sana. *** Ilikuwa saa kumi jioni, baba Mei aliingia nyumbani kwake na kulakiwa na mkewe kwa wao nyingi lakini zisizokuwa na nguvu kama inavyokuwa kawaida yake... “Vipi, za hapa mke wangu?” alisalimia baba Mei akipokewa mabegi...
“Hapa salama tu, pole na safari mke wangu.” Baba Mei baada ya kupokelewa mabegi, aliingia moja kwa moja hadi chumbani na kukaa kitandani. Hali ikaanza kubadilika kwa mama Mei. “Vipi lakini, salama hapa!” aliuliza baba Mei huku akitaka kufungua vishikizo vya shati lake. Kabla hajajibiwa, mama Mei alijiinua taratibu pale kitandani na kumshika mkono baba Mei kwa maana ya kumsaidia kufungua vishikizo.” “Salama kabisa mume wangu,” alijibu mama Mei kwa sauti ya kimahaba. “Hivi mzee Hewa yupo?” aliuliza baba Mei kwa mshangao hali iliyomshtua mama Mei kwa dakika chake kisha akajibu. ”Yupo, aende wapi tena wakati ndiyo nyumba yake hii.” “Hajaulizia kodi yake?” alisema baba Mei kwa kutania. “Hajauliza jamani, mume wangu naomba nikakuandalie maji ya kuoga,” alisema mama Mei kisha akaondoka na kumuacha baba Mei akimalizia kubadilisha nguo. Muda wote huo hadi anatoka nje, akili ya mama Mei haikuwa sawa kabisa, mawazo yake yalikuwa yakifikiria ndani ya kipindi kifupi kutembea na wanaume wawili tena nyumba moja. “Sijui, maana Mfaume alivyoniambiaga kuwa akiwa na dukuduku lazima alitoe, ananitia wasiwasi kweli na ndoa yangu,” alijisemea mama Mei. Kitendo cha mama Mei kufika bafuni na kuweka ndoo, akakutana uso kwa uso na Mfaume akiwa anatokea chumbani kwake. “Mama Mei, mama Mei?” aliita Mfaume. Mama Mei alikaa kimya, alimsikia lakini hakutaka kupoteza muda wa kukaa naye kwa kuogopa huenda yakawa yaleyale. “Mama Mei jamani si nakuita,” aliendelea kuita Mfaume, safari hii alikuwa ameshamsogelea kwa ukaribu. Akamshika begani. “Mama Mei, unaonekana una mawazo sana, nini tena mpenzi nikusaidie,” alisema Mfaume kwa sauti legevu. “Shii! Ishia hapohapo, hivi hujui kama mume wangu amesharudi?” alisema mama Mei huku akiweka kanga yake vizuri na kuondoka. Mfaume alibaki akitoa macho na mdomo wazi huku akiangalia umbo lile la mama Mei, umbo alilolifaidi usiku kucha, hakumuamini hata kidogo maneno ya mama Mei kama kweli mumewe amesharudi. Je, nini kilitokea hapo? Usikose kusoma, Ijumaa ijayo

No comments