Header Ads

Kanga Moja Kiunoni... MBENGEMBEGE - 26

 
ILIPOISHIA : “Hapana bwana, huyu mwanamke kusema ule ukweli ni matatizo juu ya matatizo... mimi ndiyo najua kila kitu. Kuaga kwangu kwamba nakwenda safari haikuwa jambo la kweli, nilitega tu,” baba Mei aliamua kufunguka... “Hodi nyumba hii,” sauti ya Jombi ilisikika akiingia... SASA JIACHIE MWENYEWE...
SAUTI ya Jombi ilionesha au kuashiria kwamba alikuwa chicha kwa pombe kwani ilitoka kwa kukatikatika. “Karibu,” Mfaume ndiye aliyeitikia hodi ya Jombi.
Wakati akipita kwenye korido, Jombi alikuwa akipepesuka na kuyumba huku akitema mate chini na kushikwa na ile hali ya kutaka kutapika, walevi wanajua... “Iiik...ikiii!” alifanya hivyo. Mbaya zaidi alikuwa ametumbukiza mikono mfukoni hivyo kuzidi kupoteza uwezo wa kujimudu kuwa imara wakati wa kutembea. “Una shida gani wewe?” Mfaume alimuuliza baada ya kumwona akiwa katika hali ile mbaya... “Kuna mtu...kuna mtu namuulizia bro,” alisema Jombi. hali aliyokuwa nayo ilimshangaza kila mtu kwani kwa muda ule wa asubuhi halafu mtu awe amelewa vile, ilikuwa kama ameamka nazo kama siyo kuzianzia mapema... “Nani?” Mfaume alimuuliza. Lakini kabla hajajibu, baba Mei alitoka akiwa amemeshika mkewe kwenye nywele akimvuta... “We ni malaya tu, huwezi kunitenda hivi hata siku moja. Mwanamke gani wewe hutulii? Hilo liumbo lako ndiyo unitese namna hii?” alikuwa akisema baba Mei. Mzee Hewa yeye alifuata mpaka sebuleni na kusimama. Alijisikia aibu kubwa kwa mtu kama Mfaume kwani walizoeana kuitana baba, mtoto. Sasa leo baba kuonekana anazini na mwanamke wa ndani ya nyumba tena binti kama wa kumzaa mwenyewe, kwa kweli aliumia sana... “Si huyu hapa, mama Mei,”
alidakia Jombi baada ya kumwona mama Mei akitoka akiwa chini ya ulinzi. Jombi hakujali kuwa, mazingira pekee yalionesha kuna tatizo, akamfuata mama Mei na kumuuliza baba Mei... “Broo kwani nini?” “Nini kuhusu nini?” baba Mei alitaka kujua akiwa amesimama kidogo. Mfaume alizidi kuwasha moto, akasema... “Huyu dogo kaja anamuulizia shemeji.” “We unamjua huyu mke wangu?” baba Mei alimuuliza Jombi...


 “Namjua, mimi nimekuja kwa ajili yake...unajua naiti moja nimewahi kupinduka ndani kwake au siyo bwana... lakini nilikuwa chenga sana sikufanya lolote...sasa samtaimu mambo kama yale ni kupanga siku mwafaka,” alisema Jomho bila woga wala simile hata kufumbafumba macho hakukuwepo. Mfaume akawa wa kwanza kubaini kuwa, mwanaume aliyemwona usiku fulani akiingia kwa mama Mei na akamwona asubuhi akitoka ni huyo... “What?” Baba Mei aliuliza kwa ukali akimaanisha nini? “Ndiyo hivyo bro,” Jombi alikazia.

 Mama Mei alikuwa kimya wakati huo akilia chini kwa chini kwani sasa ilifika hatua akawa hajui alie, anyamaze kimya au ajitetee. Baba Mei alimwingiza ndani mkewe kisha akamwita Mfaume na akamwomba amwite na mzee Hewa lakini pia akamtaka na Jombi aingie. Jombi alikuwa wa kwanza, akakaa kwenye kochi dogo pembeni ya mlango... “Ungekuja tu baba, mambo tayari yameharibika, hakuna jinsi,” alisema Mfaume akimwambia mzee Hewa... “Hapana mzee wangu, hii ni aibu kubwa sana kwangu. We unadhani mimi nitakuwa mgeni wa nani katika dunia ya watu waadilifu? Nimechafuka hivihivi najiona,” alisema mzee huyo akitokwa machozi... “Baba, kama dunia ya watu waadilifu haupo, utakutana na ile yenye daraja lako, hakuna aliyekuchafua, umejichafua mwenyewe. Lakini mimi kama mimi, lawama zangu ni kwa mwanamke... 

“Unataka kuniambia mama Mei ameshindwa kuwa na adabu kwako. Siamini kama wewe ndiyo uliyeanza kumtaka...kama ni wewe basi kuna eneo la kurekebisha mzee wangu...kwa hiyo we twende usipandishe hasira za baba Mei bure,” alisema Mfaume. Mzee Hewa aliposikia neno usipandishe hasira za baba Mei bure, mwenyewe akasimama kwani alijua anaweza kung’olewa meno. Waliingia, wakakaa... “Baba mimi sina maneno mengi sana, huyu mwanamke kuanzia leo ni wa kwenu. Wewe na huyu kijana hapa. Maana nimemuuliza kama kweli amewahi kuingia kwangu kulala amethibitisha kwa kuonesha chumba na kilipo kitanda japo amesema mengine hakumbuki kwani aliingia akiwa amelewa... “Kwa hiyo baada ya kusema hayo, mama Mei nakutaka uchukue kila chako uondoke. Amua kwenda kwa mzee huyo au kwa huyu kijana. Chaguo ni lako.

 Damu zote mbili umezipata, changa na iliyozeeka,” alisema baba Mei akisimama na kuufungua mlango ukakaa wazi. Mama Mei hakuwa na jinsi, aliingia ndani, chumbani akafungasha kila alichotaka... “Ukiweza niachie nguo zangu tu. Vitu vyote chukua, kitanda chukua, makabati chukua, makochi chukua, kila kitu, kasoro kile ambacho huwa navaa mimi... “Naweza kulala chini nikaanza upya kuliko kuwa na hivyo vitu halafu niko na wewe. Amani hakuna.” Mama Mei alishindwa kujizuia na kuanza kulia huku akisema... “Wanaume wameniponza mimi, nilikuwa nikivaa kanga moja na kutembea wanaona wowowo langu likifanya mbengembenge, wakawa wananitamani kumbe wananivunjia ndoa yangu...we mzee Hewa wewe nakulaani, hata wewe Mfaume pia umo, umeshalala na mimi.” He! Wote walishtuka, Mfaume akataka kutoka lakini baba Mei akamzuia na kumwambia awe na amani tu, kwani na yeye pia amepewa mwanamke huyo awe wake! Ama kweli, mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe! Mama Mei aliamini kule kupendwa ndiyo maisha kumbe ndiyo kujiangamiza. 
MWISHO!

1 comment: