Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge - 21

 
ILIPOISHIA  Mfaume alibaki akitoa macho na mdomo wazi huku akiangalia umbo lile la mama Mei, umbo alilolifaidi usiku kucha, hakuamini hata kidogo maneno ya mama Mei kama kweli mumewe amesharudi. SASA JIACHIE MWENYEWE... ALICHOKIFANYA alipiga hatua kama mtu anavyonyatia kwa kumfuata mama Mei kwa nyuma lakini kabla hajaufikia mlango wa mama Mei, mlango ukafunguliwa, baba Mei akachomoza. “Umeshaniwekea hayo maji bafuni?” Mama Mei akabaki na kigugumizi akijishikashika vidole huku akimwangalia Mfaume kisha akarudisha macho na kumuangalia mumewe... “Yapo tayari bafuni,” alisema. Baba Mei alishangazwa na hali ile ya mkewe, lakini hakumuuliza wala kujihoji sana mwenyewe, alijiandaa akaenda kuoga... “Nimegundua huyu
Mfaume ni kimeo naye... sasa namwambia pale halafu haamini, anatakaje?” alijisemea moyoni mama Mei. Mume wake, alikwenda kuoga, akarudi ndani na kuendelea na maisha ya nyumbani... “Mke wangu niambie, habari za hapa?” “Njema mume wangu, pole na safari...” “Nimepoa sana. vipi maisha ya siku mbili tatu?” “Maisha yapo salama baba Mei, nilikumisi sana yaani...” “Mimi je, hapa naomba jiandae uje kitandani,” alisema baba Mei huku akielekea chumbani akiwa ndani ya taulo... “Sawa mume wangu, nakuja.” Baba Mei alipofika kitandani alilala akiangalia juu. Uchovu alikuwa nao lakini pia alipenda kumpa burudani mkewe kwani ni siku kadhaa zilipita tangu aondoke. Mama Mei yeye, hakuwa kivile kwani tangu mume wake aondoke, alishadondoka na mzee mwenye nyumba na usiku wa kuamkia siku hiyo alidondoka na Mfaume. Kwa
hiyo hakuwa mhitaji sana, ila asingeweza kujionesha. Alijiandalia maji, akaenda kuoga kisha akarudi chumbani akiwa amefunga mlango mkubwa ili asitake bughudha na mtu. Alipanda kitandani mama Mei, akambusu mume wake, akamwambia anampenda sana... “Hata mimi nakupenda sana baby,” alisema baba Mei. Walishikana, wakakumbatiana, wakapigana mabusu mpaka ikafika mahali, kila mmoja akawa moto tayari kwa mpambano wa mechi. Kazi ilikuwa nzito kwa baba Mei lakini kwa uzoefu wake, hakumwona mkewe kama alimmisi sana kama inavyokuaga mara nyingi anaposafiri nje ya nyumbani kwa siku kadhaa... “Mh!” Aliguna baba Mei... “Vipi mume wangu, nini kinakugunisha?” mama Mei alimuuliza mumewe... “Hapana.” Lakini muda mwingi, baba Mei alikuwa akiguna mpaka ikafika mahali, mama Mei akaanza kuhisi kitu kutoka kwa mume wake kwamba,
amemgundua kuwa, alichepuka akiwa hayupo! Mchezo ulikwenda hivyohivyo mpaka wakamaliza dakika za uwanjani..! *** Mzee Hewa alikuwa hajui lolote kuhusu ujio wa baba Mei. Yeye alijua ni amani tu. Usiku huo hakuwa tayari kulala bila kumpata mwanamke huyo. Na alitamani sana alale naye usiku kucha akijua atakubaliwa.   Aliamka mzee Hewa, maana alishapanda kitandani kujipumzisha kama siyo kulala. Akavaa msuli wake na singilendi kwa juu, akafungua mlango na kutoka. Alitembea kwa busara zake zote ili jamii nyingine inayoishia kwenye nyumba hiyo isijue lolote. *** Kwa upande wake, Mfaume alikuwa na wakati mgumu sana. Alijua toka moyoni mwake kwamba, baba Mei aliingia shaka kwa kitendo cha kumwona yeye amesimama jirani na mke wake... “Da! Ile ishu pale haikukaa sawasawa hata kidogo. Jamaa kama ameshtukia f’lani hivi. Ila
inabidi kuwa kauzu. Kwani nini kitapotea kwangu?” alisema mwenyewe Mfaume. *** Mzee Hewa alishika kitasa cha mlango wa kwa mama Mei, akakizungusha lakini akabaini mlango huo ulifungwa kwa ndani. Akaamua kugonga. Alianza kugonga polepole mwishowe kwa sana ili asikike kule chumbani aliko... “Nani anagonga?” aliuliza baba Mei... “Mh! Sijui nani?!” mama Mei alijibu akiamini hawezi kuwa mtu anayemtafuta yeye pia akawa anajiandaa kutoka kitandani... “Ngoja niende mimi,” alisema baba Mei akitoka kitandani. Alivaa taulo, akaenda kufungua mlango huku akiwa hajui atakutana na sura gani. Kwachakwachakwacha, mlango ulifunguka. Hamadi! Sura ya baba Mei hii hapa! Je, nini kilitokea hapo? Usikose  Jumatatu ijayo.

No comments