Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge - 23

 
Mtunzi:  Irene Mwamfupe Ndauka
ILIPOISHIA : Baba Mei alimwangalia mkewe akatingisha kichwa huku moyoni akisema... SASA ENDELEA... “UNGEJUA siendi kokote na leo lazima ukweli ujulikane wala usingenitakia safari njema. Halafu utanitakiaje safari njema kabla sijaondoka? Hii inaonesha furaha yako ilipo.” *** Ilikuwa jioni ya saa kumi, baba Mei alisharudi na sasa alikuwa akiondoka zake kwa safari kama alivyomwambia mama yake asubuhi. Mama Mei alimsindikiza hadi nje kwenye gari ambako pia alikuwepo mzee Hewa na Mfaume wakiongea kabla ya Mfaume hajatoka kwenda zake kazini... “Jamani nasafiri kidogo, nitakuwa sipo kwa siku kama nne hivi,” alisema baba Mei huku macho yakiangalia pembeni kabisa kwa vile hakuwa na mazoea ya kusema uongo mkubwa kama ule. Mzee Hewa na Mfaume wakaonesha furaha ya waziwazi wakimtaka Mungu amtangulie... “Sawa bwana, safari njema, sisi tupo tu tunasogezasogeza maisha na uzee huu,” alisema
mzee Hewa akijifanya amechoka kwa umri ilimradi asifikiriwe vibaya maana, lile tukio la jana yake usiku kwenda kugonga mlango wa mama Mei kisha aliyetoka ni baba Mei akakosa cha kusema, bado lilikuwa likimtokota moyoni kwa dhamira mbaya... “Haya, nashukuru sana mzee Hewa...” “E bwana uende salama, sisi tupo kama hivi, tukitoka asubuhi hii kurudi usiku...da! hizi kazi bwana,” alisema Mfaume, naye aliamua kusema hivyo ili kujenga mazingira yenye kuweka amani kwa baba Mei. Mama Mei alisimama kwenye mlango wa gari, akawa anaongea na mumewe maneno ya mwishomwisho kabla hajaianza safari... “Nitakumisi sana darling, nitakukumbuka. Lakini nakuombea kwa Mungu, akutangulie katika safari yako, iwe njema na mwisho kabisa uhakikishe unasali kabla ya kulala ili kumwomba Mungu akulinde, lakini mwisho kabisakabisa usikose kuwasiliana na mimi mkeo ujue naendeleaje lakini mwisho kabisakabisakabisa take care,” alisema mama Mei na kumbusu mumewe...
“Mmmm...mwaaa...” “Mmm...mwaaaa...aaa,” alirudishia baba Mei, akawasha gari na kuondoka. Nje ya nyumba alikuwepo mzee Hewa tu, kwani Mfaume alishaondoka zake kwenda kazini. Na alikuwa akienda huku njiani akisema moyoni kwamba, siku ile ndiyo nzuri kwa kulala na mama Mei mpaka kunakucha kama jana yake... “Lakini jamaa namuonea kwelikweli, yaani akiwa hayupo tu, mke wake anakuwa msosi wangu...aisee mi kama ni hivi sioei. Uaminifu ni sifuri kabisa,” alisema moyoni Mfaume. *** “Sasa naona mambo mazuri,” mzee Hewa alimwambia mama Mei... “Halafu we mzee Hewa umenikera sana jana usiku,” mama Mei alikumbuka... “Kuhusu nini binti mzuri?” “We unakujaje kugonga mlango kwangu bila kuchunguza kwanza bwana...” “Mimi sikujua kama mwenye mali karudi. Usipige kelele sana binti, mishipa itapasuka bure ufe tukupoteze binti mzuri kama wewe. Ningejua mmiliki karudi hapa mlangoni nisingepita achilia mbali kugonga mlango,” mzee Hewa alisema akiingiza na
kautani kwa mbali, mama Mei akajikuta akiachia kicheko na si tabasamu... “Haya...haya...sasa unasemaje?” “Nasemaje? Jana nilikumisi sana ndiyo maana nikaja kugonga. Walahi nimelala mwili wote unauma maana sikupata usingizi nilipokuta mwenyewe yupo...” “Kwa hiyo?” “Kwa hiyo? Kwa hiyo nini sasa, si ndiyo muda wetu huu?! Paka ametoka sasa ni nafasi yangu mimi panya.” Mama Mei akacheka huku akimpa mkono mzee huyo ili agonge, akagonga waaa! “Sasa mzee Hewa?” “Nakusikiliza wewe...” “Mimi naingia ndani,” alisema mama Mei... “Na mimi nakufuata nyuma.” Kweli, mama Mei aliingia, mzee mwenye nyumba akamfuata kwa nyuma huku udenda wa mahaba ukimtoka kinywani. Mama alijua nyuma anafuatwa, alipofika kwenye usawa wa mlango wa mzee Hewa, akafungua na kuingia mwenyewe. Kitendo hicho pekee kilimfanya mzee huyo ajikute anataka kukata roho kwa tamaa...
“Da! Mpaka anatangulia mwenyewe, watu tuna bahati zetu bwana,” alisema moyoni akifuatia kwa nyuma. Mzee Hewa alijiona bado kijana mbichi kuona mwanamke kama mama Mei anamshobokea, kwake ilikuwa ngekewa ya karne. Alifunga mlango, akamkuta mama Mei amesimama katikati ya sebule. Mzigo mzigo kweli, kila idara ilikamilika. Mguu uliokanyaga chini ulishiba kwa kuumbwa...kiuno kama cha mtu wa kuchorwa, kifua ni mwanamke mwenye kujielewa, usipime bwana... “Haa! Haa!” mzee Hewa alianza kuonesha uchu wake kabisa. Alimfuata na kumkumbatia kwa kumuweka kifuani mzimamzima. Mama Mei hakutaka kuonesha kwamba, hajakubali kukumbatiwa, akatoa ushirikiano kwa yeye naye kumkumbatia... “We mama Mei,” sauti ya baba Mei iliita kwa nguvu mlangoni kwake akiwa amesimama...      Je, nini kilitokea hapo? Usikose kusoma Jumatatu ijayo.

No comments