• Latest News

  August 18, 2016

  Kijiko atenguliwa, Gambo awa RC mpya Arusha

  Bw. Mrisho Gambo.
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
  Felix Ntibenda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyetenguliwa
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
  Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mrisho Gambo Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Kijiko atenguliwa, Gambo awa RC mpya Arusha Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top