Header Ads

Kisa Sajent asutwa awekewa mpango apewe kichapo, Aingia Mitini

Mwigizaji aliyejikwaa jina kupitia Shindano la Kimwana Manywele, Husna Idd ‘Sajent’ ameiona simu yake mzigo kupitia WhatsApp baada ya kudaiwa kusutwa na baadhi ya mastaa wa kike wa Bongo Muvi katika group lao, kisa kikisemekana ni mwanaume aliyezaa na mwigizaji mwenzake, Mary Mawigi. Ubuyu kutoka kwa sosi wa kuaminika umetua kwenye kitengo chetu ukieleza mkasa mzima ambapo ilidaiwa kuwa Sajent alianzisha urafiki na Mary Mawigi huku akimpelekea maneno akimwambia kuwa mwigizaji mwenzao, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ anatembea na mwanaume huyo. Ilidaiwa kwamba, baada ya maneno hayo kumfikia Mawigi ndipo likaibuka sekeseke na kumfanya Mawigi kumchukia Kabula.
 
 Mwigizaji aliyejikwaa jina kupitia Shindano la Kimwana Manywele, Husna Idd ‘Sajent’

KISIKIE CHANZO: “Jamani ngoja niwape ubuyu ulionyooka, Sajent anasemekana kamchonganisha Mary Mawigi na Kabula akijua kabisa ni marafiki. “Ishu iko hivi; siku moja Sajent alifunga safari hadi kwa Mary Mawigi akamkalisha na kummwagia ubuyu kuwa Kabula anamlia mali zake kwa mumewe wakati akijua fika kuwa Mary Mawigi na Kabula ni marafiki. “Shosti (Sajent) alijua Mary atakuwa na kifua lakini Sajent alipompa kisogo tu, Mary akamwendea hewani baba mtoto wake na kumwambia wasijuane kuanzia siku hiyo na kusababisha songombingo. “Baada ya ‘kumlipa keshi’ mumewe, Mary Mawigi alimgeukia Kabula, akamwendea hewani na kumpa maneno mazito kwani hakuwa na kifua cha kumficha.

” MSIKIE MARY MAWIGI
Baada ya kukisikia chanzo hicho, Wikienda kama kawaida yake lilimsaka Mary Mawigi ambaye alifunguka bila kificho kwamba Sajent alimfanyia mambo ya aibu. Akisimulia kwa uchungu na hisia kali za kukwazika, Mawigi alisema alikuwa akimuamini mno Sajent kwa kila alichokuwa akimwambia, japokuwa kuna rafiki yake (jina kapuni) alimuonya asimuamini na kumtaka afanye utafiti lakini mara zote alimpinga. “Nilimuamini mno Sajent. Aliponiambia ishu ya Kabula niliumia sana. Nikamsema sana Kabula na kuchukua uamuzi wa kuachana na baba mtoto wangu.
Kumbe Sajent ndiye aliyekuwa akimtaka yeye. “Nilipombana mwanaume wangu aliniambia kuna siku Sajent alikutana naye klabu, akajifanya kulewa na kujilegeza. Vyote hivyo ilikuwa kumtia mwanaume wangu majaribuni. “Alinieleza kila kitu jinsi Sajent anavyomsumbua kwa SMS. Niliumia mno ndipo nikakubaliana na usemi kuwa kikulacho kinguoni mwako,” alisimulia Mawigi. Aliongeza kuwa, tangu siku hiyo aliamini marafiki si kila mtu ni rafiki mwema kwani Sajent alikuwa akimtumia mzazi mwenzake SMS na mbaya zaidi mwanaume yule alimuonesha ndipo alichukua uamuzi wa kuwaambia wenzake ili wamsute. “Kiukweli nilimuonea aibu Kabula kwani alikuwa akijitahidi kunielewesha siku ambayo nilimtukana kwa ajili ya mzazi mwenzangu lakini sikumuelewa. “Ukweli nimejifunza kitu, hata siku moja sitamuacha mwanaume kwa sababu ya maneno ya kusikia labda nijionee mwenyewe na sitamuamini rafiki tena. Namshukuru Mungu kwa sasa mimi na mwanaume wangu tupo poa baada ya kuweka mambo sawa,” alimalizia Mawigi.

KABULA NAYE
 Wikienda lilimsaka Kabula aliyehusishwa kwenye sakata hilo ambapo alifunguka kuwa alishangazwa na Sajent na hakuamini kama angemfanyia kitendo kama hicho kwa sababu wamejuana kitambo.

MSIKIE KABULA:
 “Hajui kwamba Mary ni ndugu yangu. Nimeshangaa kutaka kunigombanisha naye. Sema tu sikutaka kumpiga maana nilimuhurumia lakini siwezi kumsamehe kamwe ila msuto wake wa nguvu aliupata.

” SAJENT AWEKWA MTUKATI
Bila kupepesa, Ubuyu Ulionyooka ulimwendea hewani Sajent ili kuweka mzani sawa ambapo alizungumza anachokijua kuhusu msuto huo. Alipoulizwa alishangaa kwa taarifa hizo na kusema hazina ukweli na kwamba ndiyo kwanza anazisikia. Aliongeza kuwa hayo ni maneno ya  watu tu wanataka kumchafua. “Jamani mimi sina tatizo na mtu,” alisema Sajent

SOSI AKUMBUSHIA JAMBO
Pamoja na maelezo hayo, paparazi wetu alirudi tena hewani na kusisitiza kuwa Sajent asibishe lolote kwani kuna siku aliundiwa mpango wa kupewa kichapo kwenye harusi ya mdogo wake, Komediani Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ lakini aliingia mitini kwani siku ya harusi hiyo hakufika kwa madai huenda alitonywa na wambeya kuwa kingemnukia.


No comments