Header Ads

LeBron: Nataka kumiliki timu NBA

NEW YORK, Marekani
NYOTA wa kikapu katika Ligi ya NBA, LeBron James amesema kuwa ndoto yake siku moja ni kumiliki timu ambayo itakuwa ikicheza kwenye ligi hiyo ya kikapu.

Amesema anaamini moyo wake na akili yake yote inapenda mchezo huo na ndiyo maana anataka akistaafu atatakiwa kuendelea kutoa mchango wake katika kikapu kwa kumiliki timu.

Ningependa kuwa sehemu ya mmiliki au ikiwezekana mmiliki kabisa, ndoto yangu ni kumiliki timu kwa asilimia zote kisha nitaajiri rais na viongozi wengine wa juu kama ninavyotaka.

“Naamini hivyo kwa kuwa najua nina jicho la kutazama vipaji na kujua ni aina gani ya watu naweza kuwa nao, kufanya nao kazi, wawe na moyo wa kazi na wawe na uelewa,” alisema James.

Katika historia ya NBA, Michael Jordan ndiye anakumbukwa kwa kuwa mchezaji aliyepata mafanikio katika NBA kisha akamiliki timu.

Wachezaji wengine wa zamani wa NBA wamekuwa na hisa ndogo katika timu lakini Jordan yeye alikuwa bosi kabisa kwa kuimiliki timu ya Charlotte Bobcats.

No comments