• Latest News

  August 04, 2016

  Leicester wachapwa na Barcelona nchini Sweden bao 4-2

  Mchezaji ghali zaidi kununuliwa na Leicester City Ahmed Musa, aliyenunuliwa pauni milioni 16 na kuvunja rekodi ya klabu hiyo, amewafungia mabao yote mawili katika mechi ambayo wamefungwa 4-2 na Barcelona katika michuano ya Kombe la Kimataifa la Klabu.
  Munir alifungua ukurasa wa mabao kupitia pasi iliyotoka kwa Lionel Messi kabla ya nyota huyo wa Argentina muda mfupi baadaye kumuandalia pasi safi Luis Suarez aliyeongoeza la pili katika mchezo huo uliochezewa uwanja wa Friends Arena mjini Stockholm, Sweden.
  Munir aliongeza la tatu, kabla ya Musa kukomboa bao moja.
  Musa alifanikiwa kukomboa la pili lakini nguvu mpya wa Barca Rafa Mujica, mwenye umri wa miaka 17 pekee, akaifungua Barcelona la nne dakika za mwisho mwisho.
  "Msimu uliopita Leicester walishangaza sana katika soka ya Ulaya, na hii ndiyo sababu inayomfanya kila mtu kuupenda mchezo huu," meneja wa Barcelona Luis Enrique alisema baadaye.
  Lionel Messi akicheza dhidi ya Leicester CityImage copyrightGETTY IMAGES
  Image captionLionel Messi hakufunga dhidi ya Leicester lakini alichangia ufungaji wa mabao matatu ya Barca
  Mshambuliaji Jamie Vardy, aliyeongeza muda wa mkataba wake kwa miaka minne mwezi Juni, na Riyad Mahrez, ambaye amehusishwa na kuhamia Arsenal, wote walianza kwenye kikosi cha Leicester kitakachokabiliana na Manchester United katika mechi ya Ngao ya Jamii uwanjani Wembley siku ya Jumapili.
  Upande wa Barca, kando na Messi na Suarez, kulikuwa na nyota wengine kama vile Javier Mascherano na Sergio Busquets.
  Leicester wataanza kutetea taji lao la Ligi Kuu ya England dhidi ya Hull City ugenini mnamo tarehe 13 Agosti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Leicester wachapwa na Barcelona nchini Sweden bao 4-2 Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top