Header Ads

LINAH: MSIZUSHE, NIKIPATA WA ‘KU-DATE’ NAYE SITAFICHMSANII wa muziki ambaye pia anajaribujaribu kwenye uigizaji, Esterlina Sanga ‘Linah’ amesema kuwa watu wasimzushie kuhusu maisha yake ya kimapenzi kwa kuwa yeye si msiri na endapo itatokea ‘ana-date’ na mtu f’lani, atasema tu. 

Akipiga stori na paparazi wetu, Linah alisema kuwa, watu wanadai kajiweka kwa rapa Billnas lakini ukweli ni kwamba jamaa huyo ni mshikaji wake tu ambaye wanashirikiana kwenye masuala ya kimuziki. 

“Watu wanatakiwa wajue tu kuwa mimi si mtu wa kuficha uhusiano wangu, niki-date na mtu nasema tu kwamba sasa natoka na f’lani, sasa hii kunizushia kuwa natoka na Billnas haijakaa sawa,” alisema Linah ambaye sasa anafanya freshi na ngoma yake ya Raha Jipe Mwenyewe

No comments