Header Ads

LIVE KUTOKA TAIFA, AZAM MABINGWA WA NGAO KWA PENALTI 4-1

Yanga: Niyonzima anaenda kupiga ANAKOSAAAA
 
Azam: Kapombe anaenda kupiga GOOOOOO!!! Anafunga 

Yanga: Kessy anaenda kupiga penalti, ANAKOSAAAA 

Azam: Himid Mao anaenda kupiga, GOOOOOOO!!! Anafunga 

Yanga anaenda kupiga Dida GOOOOOOOOOOO Anafunga

Azam wanaanza anaanza Bocco, GOOOOOO!! Anafunga 

Dakika ya 90: GOOOOOOOOOO!!!!!!!!

Dakika ya 89Azam wanapata penaltiiiiii baada ya Kamusoko kuunawa mpira ndani ya eneo la 18.
  
Dakika ya 86: Yanga wanafanya shambulizi ngonga nzuri ya Busungu na Msuva lakini mpira unatoka.
  
Dakika ya 82: Yanga wanafanya mabadiliko, Mahadhi anatoka, anaingia Malimi Busungu.
Haruna Niyonzima anapewa kadi ya njano kutoka na kuonyesha utovu wa nidhamu kwa mwamuzi

Dakika ya 68: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Tambwe anaingia Simon Msuva.

Bocco anapiga faulo shuti linapaa juu ya lango la Yanga. 

Mchezo umesimama kwa muda, Mahadhi ameumia anatibiwa lakini Azam wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Yanga. 

Yanga wanafanya shambulizi kali lakini shuti la Kamusoko linatoka nje, wachezaji wa Azam wamzonga mwamuzi wakilalamika lakini anawapotezea na mchezo unaendelea. 

Dakika ya 57: Sure Boy anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo mchezaji wa Yanga, Haruna Niyonzima

Dakika ya 55: Kiungo wa Azam, Himid Mao anapewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Tambwe, tukio hilo limetokea katikati ya uwanja. 

Dakika ya 48: Kamusoko anapata nafasi nzuri langoni mwa Azam anashindwa kutumia vizuri nafasi hiyo kufunga. 

Azam wamefanya mabadiliko, ametoka Singano na Shaban Chilunda wameingia Mudahir Yahya na Francisco Zejumbariwa.  

Kipindi cha pili kimeanza.


MAPUMZIKO

Dakika 45: Zimeongezwa dakika mbili za nyongeza. 

Dakika ya 40: Azam wanaonekana kuamka, Mugiraneza anamiliki mpira katikati ya uwanja lakini anakuwa na kazi ngumu dhidi ya Twite. 

Dakika ya 37: Mahadi anashindwa kutumia nafasi ya wazi anayopata ndani ya eneo la 18 la Azam, anapiga shuti linapaa juu. 

Dakika ya 30: Yanga bado wanaendelea kucheza vizuri lakini Azam wanajipanga taratibu.


  

Yanga wanaongoza mabao 2-0, yote yamefungwa na Ngoma.  

  

Dakika ya 25: Azam FC wanaonekana kupoteana, mpaka sasa hawajaonyesha mchezo mzuri. Huenda mabao mawili ya haraka yamewachanganya.

GOOOOOOOOOO, Dakika ya 22, Yanga wanapata bao la pili mfungaji ni Ngoma tena, ni baada ya kuunganisha pasi nzuri ya Tambwe.

Yanga wanatawala mchezo 

GOOOOOOOOOOOOOOOOO, Dakika ya 20..Ngoma anafunga na Yanga inakuwa inaongoza bao 1-0

Ngoma anaweka kwenye kiboksi yeye mwenyewe na kupiga.

Dakika ya 19: Himid Mao anamchezea faulo Ngoma na mwamuzi anatenga tuta kuwa penaltii


Dakika ya 13: Mchezo bado 0-0, mpira umebalansi hasa eneo la katikati.John Bocco anamfanyia faulo Mbuyu Twite, mchezo umesimama kwa muda Twite akitibiwa.


Dakika ya 5: Yanga wanalishambulia lango la Azam FC, Yanga wanapata kona mbili mfulizo.


Mpira umeanza


KIKOSI CHA YANGA:
Deogratius Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Haji Mwinyi, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Said Juma, Juma Mahadhi, Thaban Kamusoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Haruna Niyonzima

Waliopo benchi ni: Benno Kakolanya, Oscar Joshua, Deus Kaseke, Simon Msuva, Malimi Busungu, Matheo Anthony, Pato Ngonyani.

  

 KIKOSI CHA AZAM FC:

Aishi Manula, Ismail Adam, Bruce Kangwa, David Mwantika, Himid Mao, Jean Mugiraneza, Shomari Kapombe, Salum Kabubakar 'Sure Boy', John Bocco, Shaban Chilunda na Ramadhani Singano.


Idadi ya mashabiki ni kubwa na taratibu wanaendelea kuongezeka.Azam wakiwasili Uwanja wa Taifa.Wachezaji wa Azam FC wakiwasili.

Tayari timu zote zimeshawasili hapa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Salehjembe itakuletea ‘live’ matangazo yote ya mchezo huo mwanzo mpaka mwisho.

No comments