• Latest News

  August 18, 2016

  MAHREZ AWAKATA MAINI BARCELONA NA MASHABIKI WAKE, ABAKI LEICESTER HADI 2020

  Na Saleh Ally, Barcelona
  Riyad Mahrez amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Leicester City ambao ni mabingwa wa Premier League na kukata mzizi wa fitna kwamba alikuwa na mpango wa kujiunga na Barcelona.

  Mahrez aliisaidia Leicester kubeba ubingwa wa England msimu uliopita akiwa amefunga mabao 17.

  Katika msimu huh, amefunga bao moja katika mechi ya kwanza ambayo walikutana na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Hull City.

  Wengi hasa katika jiji la Barcelona, waliamini leo ndiyo sikh ambayo Mahrez angetangazwa rasmi kujiunga na Barcelona.


  Lakini taariga za kwamba atabaki Leicester hadj mwaka 2020 zimewakatisha tamaa na wanaamini sasa Mahrez si anayetarajiwa kujiunga na klabu hii maarufu.

  Kumekuwa na gumzo kwamba atajiunga na Barcelona na baadhi ya makazi ya mashabiki wa Barcelona waliweka picha zake wakionyesha kusubiri kumkaribisha.

  Wengine waliandika maneno "mtoto wa nyumbani" wakiamini Algeria si mbali na Barcelona kwa maana ya eneo.

  Lakini uamuzi wake huo wa kusaini mkataba, sasa umemaliza ubishi na hisia za mashabiki hao ambao hata hivyo, kikosi chao kimejitosheleza kwelikweli.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAHREZ AWAKATA MAINI BARCELONA NA MASHABIKI WAKE, ABAKI LEICESTER HADI 2020 Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top