Header Ads

Majambazi Yaua Polisi 4 Mbande Dar es Salaam usiku wa Kuamkia Leo

ASKARI polisi wanne wameuawa  na raia wawili wamejeruhiwa kwa kupigwa  raisasi na majambazi huko Mbagala, Mbande jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB, tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka  majambazi  7 wakiwa na silaha na kuanza kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi hilo waliondoka na silaha moja aina ya SMG kwa  pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.

Imeelezwa kuwa majambazi hayo hayakuingia ndani ya benki ila gari la polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa  kwa risasi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba  akimjulia hali Raia aliyejeruhiwa
Waziri Nchemba na Kamanda Sirro wakiwa eneo la tukio
Gari ya Polisi ikiwa imezagaa Risasi

No comments