• Latest News

  August 08, 2016

  Man United ni bingwa wa FA na bingwa wa ngao ya jamii 2016...Video na Picha zipo hapa Leicester City 1-2 Manchester United

  Wiki moja kabla ya Ligi Kuu England kuanza huwa ni kawaida kuchezwa mchezo wa ngao ya jamii, mchezo ambao huzikutanisha timu Bingwa wa Ligi Kuu na Bingwa wa Kombe la FA, August 7 2016 England katika uwanja wa Wembley Leicester City ambaye ni Bingwa wa EPL na Man United ambaye ni bingwa wa FA walikutana.
  36F8DD7C00000578-3728057-image-a-56_1470588583970
  Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa mashindano kwa kocha Jose Mourinho aliyejiunga na Man United msimu huu sambamba na nyota Zlatan Ibrahimovic aliyetumia mechi hiyo kudhihirisha ubora wake wa kucheka na nyavu, katika mchezo huo Man United wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
  36FA222700000578-3728057-image-a-77_1470590473784
  Man United walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 31 kupitia kwa Jesse Lingard ila Leicester City walisawazisha goli hilo dakika ya 52 kupitia kwa mshambuliaji wao aliyeng’ara msimu uliopita Jarmie Vardy, furaha ya Leicester City ilimalizwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 83 na kuipa ubingwa wa Ngao ya Hisani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Man United ni bingwa wa FA na bingwa wa ngao ya jamii 2016...Video na Picha zipo hapa Leicester City 1-2 Manchester United Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top