• Latest News

  August 17, 2016

  Mavugo apewa nyumba Sinza jijini Dar!

  MSHAMBULIAJI wa Simba, Laudit Mavugo, pamoja na wachezaji wa kigeni waliosajiliwa Simba msimu huu, wamepangiwa nyumba maeneo ya Sinza kwa ajili ya makazi yao kwa muda wote ambao watakuwa wakiitumikia timu hiyo. 
  Mavugo ametua Simba hivi karibuni ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia klabu hiyo ambapo hadi sasa, ameshafanikiwa kufunga bao moja katika mechi ya Simba Day dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.
  Kikizungumza na Championi Jumatano, chanzo cha habari kutoka Simba kilisema, Mavugo amekabidhiwa nyumba ambayo alikuwa akiishi aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Hamisi Kiiza, ambaye amemwagwa katika usajili uliopita.
  “Mavugo na wenzie wamepatiwa nyumba maeneo ya Sinza, wachezaji wote wa kigeni wanaishi katika nyumba ambayo alikuwa akiishi (Hamisi) Kiiza ambapo huduma zote muhimu za kibinadamu zipo ndani pamoja na fenicha zote,  hivyo wao wanaishi tu.
  “Kiiza alipoondoka aliiacha nyumba ile ikiwa wazi bila kuifunga lakini tunashukuru Mungu vitu vyote tulivikuta salama, hivyo imekuwa rahisi na kuwapatia wachezaji hao wa kimataifa mahali pa kuishi,” kilisema chanzo hicho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Mavugo apewa nyumba Sinza jijini Dar! Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top