Header Ads

MIMBA YA ZARI YAIBUA BALAA, KISA KIP HAPA  Mzazi mwenzie na staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ akinyesha kuwa ni mjamzito.


Wakati ikiwa imethibitika kuwa mzazi mwenzie na staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ kuwa ni mjamzito, imedaiwa kuwa mimba hiyo hivi sasa imeibua balaa baada ya kusemwa kuwa mwanamke huyo ‘hampendi’ mwanaye, Tiffah. Chanzo cha karibu na familia hiyo kimedai kuwa Zari ana ujauzito wa mtoto wa kiume, hali inayomfanya awachukie wanawake hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kumpeleka shule mapema licha ya umri wake mdogo ili asiwe anamuona mara kwa mara.

 “Si unajua wanawake tena, wengine wakiwa na mimba ya mtoto wa kiume, wanawachukia wanawake, akiwa nayo ya kike, anawachukia wanaume, sasa ndivyo ilivyo kwa Zari hivi sasa anaona kama uwepo wa Tiffah karibu yake haumpi furaha, ndiyo maana a m e a m u a kumpeleka shule bintiye huyo huko Afrika Kusini wanakoishi,” kilisema chanzo hicho. 

“Yaani mimba inamsumbua sana Zari huku Tiffah akiwa bado mdogo maana si unajua watoto wadogo wanakuwa na fujo wakati mwingine, sasa ukichanganya fujo na usumbufu huo, ndiyo maana ameamua kumpeleka shule hali ambayo imempunguzia usumbufu kiasi,” kilisema chanzo. “Zari na Diamond kipindi hiki wanagombanagombana kidogo, nafikiri ni kwa sababu ya hiyo mimba maana hata kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, mara nyingi amekuwa akiweka picha zake na watoto wake.

 “Lakini Diamond yeye kwa kuwa ameshajua tatizo la mwenzake, anaweka picha za Zari kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akimsifia lakini mwanamama huyo hafanyi hivyo kama ilivyokuwa zamani,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kuzipata habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Diamond ambaye alipopatikana, alisema haoni tatizo kwa mtoto kupelekwa shule katika umri huo, kwa sababu ni utamaduni wa nchi zilizoendelea kutokana na ubize wa wazazi na pia ubora wa vituo vya kuwaangalia watoto hao. “Uangaliazi wa watoto katika shule hizo (Day Care) ni mkubwa, hamna tatizo, hayo mambo mengine miye sijui kwa sababu tupo safi tu,” alisema

No comments