Header Ads

Mkongo siri nje! Wema anadaiwa kutoka kimapenzi na Radjabu Mwami mpenzi wa zamani wa Wolper, Husna Maulid, Tunda Sabasita na Hamisa Mabeto

Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye uhusiano wake wa kimapenzi na Idris Sultan umeingia katika sintofahamu, siri zimevuja nje kuwa mrembo huyo mwenye mvuto, hivi sasa anatoka kimalovee na jamaa ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayetajwa kwa jina la Radjabu Mwami. 

Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wanadaiwa kutoka kimapenzi kwa siri, ingawa mara zote wamekuwa wakikanusha jambo hilo. Kwa mara ya kwanza, picha zilizonaswa na Wikienda zikiwaonesha wawili hao wakiwa wamepozi kimahaba zimezidisha uvumi huo ambao kwa sasa ndiyo habari ya mjini. 

“Mimi najua, ingawa ni vigumu watu kuamini, hawa wanatoka. Sijui mastaa wa Bongo huwa wanafuata nini kwa huyu Mkongo maana naona anawapanga tu foleni dada zetu wa Kibongo, si unajua ameshatembea na wasichana wengine mastaa kibao?” kilisema chanzo hicho. Mwami anahusishwa kutoka kimapenzi pia na mastaa wengine kama Jacqueline Wolper Massawe, Husna Maulid, Tunda Sabasita na Hamisa Mabeto. 

Baada ya kuunasa ubuyu huo, gazeti hili liliwatafuta wawili hao, wa kwanza kupatikana akiwa ni Mwami ambaye anatajwa kuwa ni mfanyabishara nchini. Alipoulizwa kinachoendelea kati yake na Wema, hasa kwa picha zilizonaswa alijibu: 

“Ninawashangaa sana ninyi, kwa nini kila siku mnashughulika na habari zangu, kwani hamna kazi nyingine ya kufanya? Sasa kupiga picha kama hiyo na mtu unayefahamiana naye kuna tatizo gani? Hizo habari za kimapenzi mnajua ninyi mimi sielewi lolote.” Kwa upande wake, Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno uliomwelezea tuhuma dhidi yake hakujibu.

No comments