Header Ads

Modo maarufu Vera Sindika alia kuambiwa ana Ukimwi!Ubuyu unaotrendi mjini ni bifu matata la mamodo wawili wa Afrika Mashariki kutoka nchini Kenya ambao hupatikana Bongo mara kwa mara, Vera Sindika na Huddah Monroe. Vera ni video queen na Huddah ambaye ni mshiriki wa Big Brother Africa, wote ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii kutokana na tabia zao za kutumia mapichapicha yenye kuteka hisia za wanaume hivyo kuwa na ‘wafuasi’ wengi mitandaoni. 


Inadaiwa kuwa, kabla ya kutibuana kwao, Vera na Huddah waliwahi kuwa mashosti wakubwa huku Vera akiwa queen wa Mombasa na Huddah akijijengea himaya kwenye Jiji la Nairobi. Bifu lao linaelezwa kuanza mara baada ya Vera kuhamia Nairobi ambapo ilidaiwa kwamba, Huddah hakupendezwa na kitendo hicho kwa madai kuwa Vera angemchukulia mabwana zake kutokana na umbo lake tata. 

Pia kuna skendo kuwa, mbali na kudaiwa kujiuza kwa bei mbaya kwa wanaume matajiri huko Dubai na Nigeria, waliwahi kuhusishwa na suala la usagaji kabla ya kuvunjika kwa ushosti wao. Vera na Huddah wanadaiwa kuwa na utajiri mkubwa wenye maswali kutokana na shughuli wanazozifanya za burudani ambapo huwa wanalipwa kwa kutokezea kwenye tukio la kiburudani. Yaani kitendo cha kufika tu na kuonekana, kwao ni fedha ndefu.

 KWA NINI HAWAKAUKI BONGO? Inasemekana kwamba, Vera na Huddah huwa hawakauki Bongo kwa sababu wana uhusiano wa karibu na baadhi ya mastaa na wafanyabiashara matajiri. Hivi karibuni walipata umaarufu zaidi kutokana na ukaribu wao na mwandani wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambao kwa pamoja huandaa shoo za White Party kwa Afrika Mashariki. 

VERA ATANGAZIWA ANA UKIMWI Ilidaiwa kwamba kwa sasa mambo si mambo kati ya warembo hao kufuatia Vera kueleza namna ambavyo Huddah amekuwa akimtoa chozi kwa kumtangazia kwamba ni mwathirika wa Ugonjwa wa Ukimwi a.k.a Ngoma. Lakini wiki iliyopita ubuyu huo ulinoga baada ya Vera ambaye yupo Bongo kuamua kufunguka kilicho ndani ya mtima wake akidai kwamba, Huddah amekuwa na roho ya kwa nini anapomuona Vera akifanya kitu kizuri. 

MSIKIE VERA: “Unajua kinachotokea ni kwamba, mimi nikifanya kitu kizuri inakuwa shida kwake (Huddah), sijawahi kuelewa ni kwa nini? “Ni miaka mine sasa tangu Huddah ameanza kunisema kuwa mimi ni mgonjwa, nina Ukimwi. “Kuna wakati ilibidi niweke video kwenye Snapchat (mtandaoni wa kijamii). Nilisema kuwa amesema mimi nina Ukimwi? Leo nitapima mtaona damu yangu ikitoka ikionesha kweli nina Ukimwi au sina. “So nikafanya test (vipimo) nikaweka video ya tukio zima kwenye Snapchat yangu, watu wakaona kweli niko negative (hana Ukimwi), basi yeye akaonekana anadanganya. “Unajua kufanya hivyo (kumtangazia mtu ana Ukimwi) ni kumharibia mtu jina kwa sababu kila time (wakati) akisema hivyo, mitandao ya kijamii inaandika, sasa niliona nimechoka ndiyo maana nikaona niweke mambo hadharani. “Kwa sasa nina zaidi ya miaka minne sijakutana na Huddah uso kwa uso lakini suala la kunitangazia mimi na ndugu zangu tuna HIV/ AIDS linaniuma sana.

” HUDDAH ANASEMAJE? Kwa upande wake, Huddah, katika mahojiano na vyombo vya habari vya Kenya juu ya ugomvi na Vera alijibu kwa kifupi: “Wengi hawafahamu kuwa ukaribu wangu na Vera umekuwepo tangu zamani. Chuki baina yetu imekuwa ikisukumwa na vyombo vya habari pamoja na baadhi ya watu. “Chuki ni hisia dhaifu. mimi na Vera tuna historia ya vitu vingi tulivyowahi kufanya pamoja. Nampenda sana, sema tu tofauti zetu zimekuwa zikichochewa na baadhi ya watu ambao hawapendi kuona amani ikitawala kati yetu.”

No comments