Header Ads

Mume wa Kajala kupambana na waliochepuka na mkewe wakati akiwa gerezani

 
Baada ya mume wa muigizaji Kajala Masanja, Faraji Chambo kufutiwa mashtaka ya kubadilisha umiliki wa nyumba iliyokuwa na zuio la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), ubuyu mpya unadai kuwa, mume huyo anapanga kutumia nguvu kubwa kukabiliana na kesi yake iliyosalia na akifanikiwa kutoka uraiani, atawashughulikia wote waliochepuka na mkewe wakati akiwa gerezani. Hukumu ya rufaa hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mahakama ya Rufaa Tanzania chini ya jopo la majaji watatu; jaji Bernard Rwanda, Batuel Mmila na Richard Mziray ambao walifuta adhabu ya kifungo cha miaka saba na faini ya shilingi milioni 213 dhidi yake. Kwenye hukumu hiyo iliyotolewa Machi mwaka 2013, licha ya Faraji, mkewe huyo ‘aliponyoka’ kwenye kifungo cha miaka 5 baada ya kulipiwa faini ya shilingi milioni 13 ambazo zilitolewa na shosti yake, Wema Sepetu ‘Madam’. 
 

Kwa mujibu wa mtoa taarifa aliye karibu na ndugu wa Faraji, jamaa huyo alikuwa akipata taarifa za wanaume mbalimbali ambao walitumia nafasi ya yeye kuwa jela, kumrubuni mkewe Kajala hivyo atakula nao sahani moja mmoja baada ya mwingine. “Jamaa alikuwa anapewa habari akiwa kule gerezani, moyo wake ulikuwa unamuuma sana. Unajua Kajala ni mwanamke wake aliyempenda kuliko maelezo, hivyo alikuwa akiahidi mara kwa mara kwamba siku akifanikiwa kutoka gerezani, lazima aonane na wote waliochepuka na mkewe. “Sasa kwa kuwa kuna dalili za kurudi, amesema
atahakikisha kwanza anajiridhisha kwa kila aliyetajwa
kama ni kweli alitembea na mkewe na kila atakayemuuliza, akileta za kuleta amesema anajua cha kumfanya na kamwe hatasahau maana nao hawakumfanyia ubinadamu,” kilisema chanzo hicho. Miongoni mwa watu ambao wanatajwa kuchepuka na Kajala na habari zao kuchorwa gazetini ni pamoja na mastaa wa Bongo Fleva; Nasibu Abdul ‘Diamond’, Quick Rocka, Msami Baby na kigogo maarufu kwa jina la CK. Gazeti hili lilimtafuta Kajala kutaka kujua maoni yake kufuatia hukumu hiyo, alipopatikana alisema awali haikuwa rahisi kwake kuamini, lakini anamshukuru Mungu kwa kilichotokea ingawa alisema mumewe hawezi kutoka gerezani kwa vile ana kesi nyingine inayomkabili, ambayo haina dhamana. “Kinachoendelea hapa kwangu kwa sasa ni kufuatilia utaratibu wa kuweza kuzipata hizo fedha ila nasikitika sana mume wangu hawezi kutoka gerezani kwa sasa kwa sababu ana kesi nyingine,” alisema Kajala. Licha ya kutumikia kifungo chake cha miaka 7 jela, Chambo pia ana kesi nyingine ya utakatishaji fedha ambayo haina dhamana


CHANZO IJUMAA WIKIENDA

No comments