Header Ads

Muonekano Mpya Wa Ijumaa wapagawisha wasomaji Kisarawe!

1Muuzaji wa magazeti ya Global, Mwamvita Rashid (kushoto) akiwauzia wasomaji wa Gazeti la Ijumaa.
2Salome Elias (kulia) akilisoma gazeti la Ijumaa baada ya kununua kwa Mwamvita.
3Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (kulia) akimwelekeza jambo msomaji wa Ijumaa.
4Benjamini Paul (kushoto) akifafanuliwa jambo na Mkanda baada ya kufungua gazeti lake.
5Mkanda (katikati) akiwapa maelekezo wasomaji wa Gazeti la Ijumaa.
6Wasomaji wa Ijumaa, Jacqueline Lwiza na Zainabu Yahya (wa pili kulia) wakisaidiwa kutoa pini za gazeti hilo.
7Wasomaji wa Ijumaa wakiendelea kupata ufafanuzi wa jambo baada ya kulinunua Gazeti la Ijumaa.
8
Msomaji wa Ijumaa, Mayasa Ramadhan (katikati) akimwonesha baadhi ya kurasa zenye hadithi anazopendelea kusoma ndani ya gazeti hilo.
9Mohamed Musa mkazi wa Kisarawe (katikati) akilisoma gazeti la Ijumaa.
10
Msomaji wa Ijumaa mkazi wa Kisalawe, Fred Kapinga (katikati) akilisoma gazeti lake.
11
Simon Isaya akilisoma gazeti la Ijumaa. Anayemshuhudia (kushoto) ni Ofisa Usambazaji wa Global, Jimmy Haroub.
12
Harakati za hapa na pale zikiendelea kwa wasomaji hao.
1314
Wasomaji wakipozi na Gazeti la Ijumaa.
 GAZETI la jumaa lenye muonekano mpya jana lilionekana kuwa kivutio kikubwa baada ya wasomaji wake wa Kisarawe mkoani Pwani kuchangamkia kulinunua huku wengi wakisema wanalikubali kwa habari zake za burudani na michezo.
Timu ya gazeti hilo ilitinga eneo hilo kuanzia asubuhi na kuzunguka sehemu mbalimbali ambapo wadau kibao walionekana wakiwa wamelinunua na wakaeleza kuwa, wanakubali mabadiliko yaliyofanyika.
Walisema kuwa, kinachowavutia zaidi ni habari na makala mbalimbali zinazowahusu mastaa ambazo zinawafanya wasuuzike na roho zao wanapolisoma.
“Kwa kweli Ijumaa ndiyo gazeti bora Bongo, habari zake na makala ni burudani tosha hasa ukichukulia kwamba ndilo linaloandika habari za mastaa kwa undani,” alisema Salome Elias.
Akizungumza na wakazi eneo hilo, Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers inayozalisha gazeti hilo pamoja na Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, na Championi, Yohana Mkanda aliwaomba wasomaji wa magazeti hayo kuendelea kulinunua Ijumaa kwa bei ya Sh.1,000 kwani thamani ya kilichomo ndani yake ni zaidi na bei hiyo.
(HABARI/PICHA:  DENIS MTIMA/GPL)

No comments